• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Rukwa Region
Rukwa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Rukwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Sumbawanga
    • Wilaya ya Nkasi
    • Wilaya ya Kalambo
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Nkasi
    • H/Wilaya ya Kalambo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Utalii
    • Madini
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Miundombinu ya Rukwa
  • Huduma zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Livestocks
    • Huduma za Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Huduma za Kisheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Fedha
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
    • Waliofaulu na Waliochaguliwa Shule

Makamishna Wa Ardhi Watakiwa Kukutana Na Taasisi Zinazodaiwa Kodi Ya Pango La Ardhi

imewekwa Tar: June 30th, 2020

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula amewaagiza Makamishna Wasaidizi wa ardhi katika ofisi za mikoa kukaa na taasisi za serikali zinazodaiwa kodi ya pango la ardhi kuangalia namna bora ya kulipa madeni wanayodaiwa.

Dkt Mabula alitoa agizo hilo jana mkoani Rukwa wakati akizundua rasmi ofisi ya ardhi ya mkoa ikiwa ni mfululilizo wa uzinduzi wa ofisi za ardhi katika mikoa mbalimbali nchini. Tayari ofisi saba za ardhi katika mikoa ya Tanga, Arusha, Manyara, Singida, Iringa, Njombe na Songwe zimezinduliwa.

Alisema, mkoa wa Rukwa una taasisi za serikali pamoja na watu binafsi ambao kwa ujumla wao wanadaiwa zaidi ya shilingi bilioni moja kiasi alichokieleza kuwa ni kikubwa na fedha yake ingeweza kutumika katika shughuli za maendekeo kama vile ujenzi wa hospitali au barabara.

Alizitaja baadhi ya taasisi za serikali zinazodaiwa kodi ya pango la ardhi katika mkoa wa Rukwa kuwa ni pamoja na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) na Chuo Kikuu Huria na kubainisha kuwa katika kumuwezesha rais kufanya kazi ya shughuli za maendeleo kuna wajibu wa kulipa kodi ya pango la ardhi.

‘’Bilioni moja ni fedha nyingi sana nawaagiza Makamishna Wasaidizi wa mikoa kukutana na taasisi pamoja na watu wengine wanaodaiwa kodi ya pango la ardhi kukubaliana namna bora ya kulipa fedha wanazodaiwa vinginevyo taratibu za kisheria zitafuata’’ alisema Dkt Mabula

Kwa mujibu wa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Taasisi za serikali zinatenga fedha kwenye bajeti zake kwa ajili ya kulipia gharama mbalimbali ikiwemo kodi ya pango la ardhi na kutolipa kodi hiyo ni kutotimiza wajibu wa kulipa kodi ya ardhi.

Alisema, Wizara yake ilikutana na makampuni na taasisi za serikali zenye malimbikizo makubwa ya kodi ya pango la ardhi mkoani Dodoma na baada ya kukutana ndani ya mwezi mmoja zilikusanywa takriban bilioni ishirini na moja jambo linaloonesha kuwa taasisi hizo zinazo fedha kwa ajili ya kodi hiyo.

Matangazo

  • Orodha ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga Kidato cha Kwanza Mwaka 2021, Mkoa wa Rukwa December 18, 2020
  • Fomu za Kujiunga na Shule mbalimbali za Sekondari (JOINING INSTRUCTION) kwa Mwaka 2021 mkoani Rukwa. December 20, 2020
  • UTARATIBU WA UOMBAJI WA VITAMBULISHO VYA UJASILIAMALI March 24, 2021
  • Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) October 09, 2018
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • Serikali ipo inafanya kazi vizuri na itaendelea kuwepo, muhimu kudumisha amani – RC Wangabo

    April 05, 2021
  • Wananchi watakiwa kuacha kulalamika na badala yake waisaidie serikali ili kuijenga nchi.

    March 07, 2021
  • RC Wangabo atoa elimu ya kujikinga na majanga huku nyumba Zaidi ya 80 zikiezuliwa na upepo

    March 06, 2021
  • Mpango wa Mji wa Sumbawanga Kupata maji kutoka Ziwa Tanganyika unakaribia.

    March 02, 2021
  • Angalia Zote

Video

Mwaka 2020 kuwa mwaka wa kuwalinda watoto dhidi ya Ukatili Mkoani Rukwa
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Miundombinu ya Rukwa
  • Uvuvi
  • Mikakati ya Mkoa
  • Industries
  • Madini
  • Speeches
  • Huduma za Kilimo
  • Regional History
  • Hotuba

Viunganishi Linganifu

  • Pakua Salaryslip yako hapa
  • Idara ya Takwimu (NBS)
  • Kilio cha Wananchi kinasikilizwa
  • Watumishi portal
  • Tafuta ajira Serikalini
  • Pata kila kitu kutoka serikalini

World visitors tracker

world map hits counter

Wapitiaji

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

    Regional Block, 90 Mwl. Julius Nyerere Road

    Sanduku la barua: Box 128 Sumbawanga

    Simu: 025 280 2137

    Simu: 0756941328

    barua pepe: ras@rukwa.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa