• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Rukwa Region
Rukwa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Rukwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Sumbawanga
    • Wilaya ya Nkasi
    • Wilaya ya Kalambo
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Nkasi
    • H/Wilaya ya Kalambo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Utalii
    • Madini
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Miundombinu ya Rukwa
  • Huduma zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Livestocks
    • Huduma za Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Huduma za Kisheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Fedha
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
    • Waliofaulu na Waliochaguliwa Shule

Rukwa waanza kuboresha taarifa za wapiga kura wa uchaguzi mkuu

imewekwa Tar: May 3rd, 2020

Mkoa wa Rukwa leo tarehe 2.5.2020 umeungana na baadhi ya mikoa mingine katika kutekeleza awamu ya pili ya zoezi la kuboresha daftari la kudumu la mpiga kura ambapo awamu hii utafanyika katika ngazi ya vituo vya kata ikiwa ni hatua za tahadhari ya kupambana na ugonjwa wa homa kali ya mapafu unaosababishwa na virusi vya Corona (Covid-19)

Hayo yamesemwa na Afisa Serikali za Mitaa Albinus Mgonya wakati akitoa salamu zake katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri kilichohusu utekelezaji wa hoja za ukaguzi na mapendekezo ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali nchini, ambapo alisema kuwa zoezi hilo litakamilika tarehe 4.5.2020.

Mgonya alisema kuwa zoezi hilo la kuboresha daftari la kudumu litakwenda sambamba na uwekaji wazi wa daftari la awali la wapiga kura waliojiandikisha katika uboreshaji wa awamu ya kwanza na kuongeza kuwa uwekaji wazi huo unapatikana katika vituo vyote ambapo mwananchi alijiandikisha katika vituo vilivyokuwa vimeainishwa na halmashauri.

“Mheshimiwa Mwenyekiti lengo la hatua hii ni kuwapa fursa wananchi waliojiandikisha awali ili waweze kuhakiki taarifa zao, kwa maana ya kwamba kama majina yamekosewa au na taarifa nyingine kadiri itakavyobidi,” Alisema.

Aidha aliwaweka wazi wahusika wa zoezi hilo kuwa ni wananchi waliotimiza umri wa miaka 18 na kuendelea ambao hawakupata fursa ya kujiandikisha awali,  watakaotimiza umri wa miaka 18 ifikapo Oktoba, 2020, waliojiandikisha na kuhama kata ama jimbo, wananchi wenye taarifa au majina yaliyokosewa wakati wa uandikishaji, waliopoteza kadi zao ama kuharibika.

Halikadhalika aliweka wazi utaratibu wa kuendesha zoezi hilo kwa kuzingatia hatua zote za kiafya zinazotakiwa kuchukuliwa wakati wa kutekeleza zoezi hilo ikiwa ni pamoja na kituo kuwa wazi na chenye nafasi ya kutosha ili kutoruhusu msongamano.

Matangazo

  • Matokeo ya Darasa la Saba 2019 - Rukwa October 17, 2019
  • Orodha ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga Kidato cha Kwanza Mwaka 2021, Mkoa wa Rukwa December 18, 2020
  • Fomu za Kujiunga na Shule mbalimbali za Sekondari (JOINING INSTRUCTION) kwa Mwaka 2021 mkoani Rukwa. December 20, 2020
  • Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) October 09, 2018
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • Wananchi wasisitizwa kuitumia wiki ya sheria kama fursa ya mafunzo ya bure ya sheria.

    January 24, 2021
  • MABARAZA YA ARDHI YATAJWA KUWA CHANZO CHA MIGOGORO

    January 23, 2021
  • Kamati ya Amani Rukwa yamuomba RC kufikisha salamu zao kwa Rais Magufuli.

    January 22, 2021
  • Kijiji kitakachokaribisha “Lambalamba” Kuwekwa chini ya Ulinzi

    January 21, 2021
  • Angalia Zote

Video

Mwaka 2020 kuwa mwaka wa kuwalinda watoto dhidi ya Ukatili Mkoani Rukwa
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Miundombinu ya Rukwa
  • Uvuvi
  • Mikakati ya Mkoa
  • Industries
  • Madini
  • Speeches
  • Huduma za Kilimo
  • Regional History
  • Hotuba

Viunganishi Linganifu

  • Pakua Salaryslip yako hapa
  • Idara ya Takwimu (NBS)
  • Kilio cha Wananchi kinasikilizwa
  • Watumishi portal
  • Tafuta ajira Serikalini
  • Pata kila kitu kutoka serikalini

World visitors tracker

world map hits counter

Wapitiaji

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

    Regional Block, 90 Mwl. Julius Nyerere Road

    Sanduku la barua: Box 128 Sumbawanga

    Simu: 025 280 2137

    Simu: 0756941328

    barua pepe: ras@rukwa.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa