• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Rukwa Region
Rukwa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Rukwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Sumbawanga
    • Wilaya ya Nkasi
    • Wilaya ya Kalambo
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Nkasi
    • H/Wilaya ya Kalambo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Utalii
    • Madini
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Miundombinu ya Rukwa
  • Huduma zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Livestocks
    • Huduma za Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Huduma za Kisheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Fedha
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
    • Waliofaulu na Waliochaguliwa Shule

Viongozi wa Dini Rukwa kupewa mbinu za kukabiliana na ukatili dhidi ya watoto

imewekwa Tar: January 1st, 2020

Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amesema ili kukabiliana na ukatili dhidi ya watoto, serikali haina budi kufanya kazi kwa karibu na viongozi wote wa dini wa madhehebu mbalimbali katika mkoa huo ikiwemo kuwataka kuwa karibu na watoto ili watoto hao wawe huru kuwataarifu viongozi hao aina yoyote ya manyanyaso wanayoyapata wakiwa nyumbani.

Amesema kuwa kwa muda mrefu katika mkoa watoto wamekuwa wakiathirika kutokana na ugomvi baina ya wazazi na hatimae kutopata mapenzi ya baba na mama hali inayopelekea watoto hao kutopata malezi mazuri ya kifamilia na hatimae kuishia mitaani na kuwa na kizazi kisichofaa katika jamii na kusisitiza kuwa serikali ya mkoa imejizatiti kupambana na hali hiyo.

“ Chimbuko la maisha yetu wote liko kwenye familia na familia ni watoto, kwahiyo tujielekeze zaidi katika malezi ya watoto wetu, lakini pia kuhakikisha ya kwamba tunawapa na kuheshimu haki zao, haki za watoto tunakwenda kuzifungua kwa watoto wetu wote kama serikali, tutawaelimisha watoto haki zao, tutawaambi wakifanyiwa manyanyaso waende kwa nani, waripoti kwa nani matatizo hayo,” Alisema

“lakini narudi kwa viongozi wa dini na wenyewe tutawaomba wawe karibu sana na watoto ili watoto waweze kufunguka wawaambie manyanyaso wanayoyapata majumbani, nasi tutashirikiana na viongozi wa dini kupambana na hayo manyanyaso na huo ukatili wa watoto” Alisisita.

Mh. Wangabo ameyasema hayo alipokuwa akitoa salamu zake za mwaka mpya katika ibada ya kuukaribisha mwaka 2020 iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Kristu Mfalme, mjini Sumbawanga.

Mwishoni mwa mwaka 2019 ofisi ya mkuu wa mkoa wa Rukwa ulizindua mpango mkakati wa wa miaka mitano wa kukabiliana na kupambana na mimba za watoto pamoja na kupunguza watoto wa mitaani, mpango ambao utekelezaji wake unaanza mwaka 2020.

Matangazo

  • RATIBA YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE August 20, 2025
  • RATIBA YA MTIHANI WA UPIMAJI WA KIDATO CHA PILI 2025 November 05, 2025
  • RATIBA YA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI 2025 August 20, 2025
  • MATOKEO YA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI 2025 November 05, 2025
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • MKUU WA MKOA WA RUKWA ATOA WITO KWA WANANCHI KUJITOKEZA KUPIGA KURA OKTOBA 29, 2025

    October 27, 2025
  • JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI RUKWA LAPOKEA MAGARI MATATU YA KISASA KUIMARISHA SHUGHULI ZA UOKOAJI

    October 27, 2025
  • SERIKALI YATOA PIKIPIKI KWA MAAFISA MAENDELEO YA JAMII WA HALMASHAURI RUKWA

    October 24, 2025
  • MBIO ZA MWENGE ZAENDELEA KALAMBO RUKWA, MIRADI YA MAENDELEO YAENDELEA KUMULIKWa

    September 30, 2025
  • Angalia Zote

Video

LIVE- WAZIRI MCHENGERWA ANATAO TANGAZO LA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Miundombinu ya Rukwa
  • Uvuvi
  • Mikakati ya Mkoa
  • Industries
  • Madini
  • Speeches
  • Huduma za Kilimo
  • Regional History
  • Hotuba

Viunganishi Linganifu

  • Pakua Salaryslip yako hapa
  • Idara ya Takwimu (NBS)
  • Mfumo wa Kutuma, Kupokea na kufuatilia Malalamiko, Mapendekezo, Maulizo na Pongezi
  • Watumishi portal
  • Tafuta ajira Serikalini
  • Pata kila kitu kutoka serikalini

World visitors tracker

world map hits counter

Wapitiaji

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa