Kuanzia Tarehe 30 Mei, 2019 kuna taarifa zilizosambaa na kutolewa na baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuhusu mama mjamzito anayesemekana kujijeruhi maeneo ya tumboni na kupelekea kutoa mtoto tumboni, tukio lililotokea kata ya kirando halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa. Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt. Boniface Kasululu anaelezea kisa kamili
Mkuu wa Mkoa wa rukwa Mh. Joachim Wangabo ameeleza tukio la vifo vya watoto wawili kwa masikitoko makubwa, tukio lililohusishwa na imani za kishirikina katika Mkoa huo na kutoa pole kwa wafiwa wa mtaa wa Vuta, Kata ya Kizwite Sumbawanga Mjini.
Katika kuelekea siku ya upandaji miti kimkoa ambayo hufanyika kila tarehe 19 ya mwezi wa kwanza kila mwaka Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amewaasa wananchi pamoja na taasisi mbalimbali za kiserikali na zisizo za kiserikali kufika katika ofisi za wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) ili kuweza kupatiwa miche ya miti na kuweza kuipanda katika maeneo yao.
Amesema kuwa TFS wametenga miche 100,000 kwaajili ya kutoa bure kwa taasisi pamoja na wananchi ambao watachangia kiasi cha shilingi 150 kwa mti mmoja na kuongeza kuwa kuchukua miti hiyo na kuipanda kutaiwezesha taasisi ama mwananchi kuwekeza katika miti, kupendezesha eneo lake hali itakayopelekea kupendezesha mandhari ya mkoa kwa ujumla.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa