Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amekutana na Kaimu Balozi wa Marekani nchini Inmi Patterson na kujadili vipaumbele vya mkoa wa rukwa na kuona namna ubalozi wa marekani utakavyoweza kuusaidia mkoa katika kufanikisha vipaumbele hivyo hasa katika sekta ya kilimo, Elimu na Lishe.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amevionya vikundi vya kidini vinavyoanzishwa baada ya kutokea migogoro kwenye makanisa na misikiti kufuata sheria katika kufanya shughuli zao za kiibada na sio kujianzisha kiholela.
Amesema kuwa kila mtanzania ana uhuru wa kuabudu akiwa mmoja lakini linapokuja suala la kikundi basi hakuna budi kikundi hicho kifuate taratibu za kujisajili ili kiweze kutambulika na vyombo vya serikali kwani vyombo vyote vya kidini vinatambulika kisheria na vimesajiliwa.
Ntembwa Falls - Nkasi, Rukwa.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa