Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt. Boniface Kasululu ametoa elimu ya kina juu ya uzambazwaji wa ugonjwa hatari wa kipindupindu ulioua na kuathiri zaidi ya watu 500 ndani ya kipindi cha miezi sita. Ameyasema hayo katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika kambi ya Nankanga Bonde la Ziwa Rukwa.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa mh. Joachim Wangabo amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa kuanzisha mchakato wa kinidhamu na uchunguzi mara moja dhidi ya Mkurugenzi wa Halamashauri ya Wialaya ya Kalambo kutokana na utendaji kazi wake usioriddhisha.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh.Joachim Wangabo amefafanua sababu kadhaa zilizosababisha Mkoa wa Rukwa kuongoza kwa utoro katika hotuba ya Waziri Mkuu Mh. Kasim Majaliwa alipokuwa akizindua mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoani Geita mapema mwezi huu.
Pia ameeleza mikakati kadhaa ya kukabiliana na utoro huo ikiwemo kusimamia programu ya chakula kwa wanafunzi ili kuwawezesha kuwa na moyo wa kusoma wawapo mashuleni.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa