WITO KWA WAFANYABIASHARA NDOGONDOGO
Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum inawakaribisha wafanyabiashara wadogondogo nchini kuchangamkia fursa ya mikopo yenye riba nafuu ya asilimia 7 kwa mwaka, inayotolewa kupitia Benki ya NMB chini ya usimamizi wa Serikali.
Mikopo hiyo inalenga kuwawezesha kiuchumi wafanyabiashara wenye mauzo yasiyozidi shilingi milioni 4 kwa mwaka, kwa lengo la kuongeza mitaji, kukuza biashara na kuboresha maisha yao.
Masharti makuu kwa waombaji ni:
1. Awe mfanyabiashara mdogondogo,
2. Awe amesajiliwa katika mfumo wa WBN–MIS.
Wafanyabiashara wote wenye sifa wanahimizwa kutembelea Ofisi za Maendeleo ya Jamii katika Kata au Halmashauri zilizo karibu nao kwa ajili ya kupata maelezo zaidi na kukamilisha taratibu za usajili.
Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, inaendelea kutekeleza mikakati ya kuwawezesha wananchi kiuchumi kwa lengo la kujenga Taifa lenye usawa, ustawi na maendeleo endelevu.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa