• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Rukwa Region
Rukwa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Rukwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Sumbawanga
    • Wilaya ya Nkasi
    • Wilaya ya Kalambo
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Nkasi
    • H/Wilaya ya Kalambo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Utalii
    • Madini
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Miundombinu ya Rukwa
  • Huduma zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Livestocks
    • Huduma za Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Huduma za Kisheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Fedha
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
    • Waliofaulu na Waliochaguliwa Shule

Maadili ya Msingi

KANUNI ZA MAADILI YA UTENDAJI KATIKA UTUMISHI WA UMMA

Kanuni hizi zimetungwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Manejimenti ya Utumishi wa Umma kwa mujibu wa Mamlaka aliyopewa katika Kifungu cha 34 cha Sheria ya Utumishi wa Umma ya Mwaka 2002 pamoja na Kanuni ya 65 (1) ya Kanuni za Utumishi wa Umma za Mwaka 2003.

 

Kutoa Huduma Bora

Watumishi wa Umma wanapaswa kutambua kwamba wana wajibu wa kutoa huduma bora kwa Umma. Katika kutimiza wajibu wao, wanapaswa pia kuzingatia yafuatayo:-

  • Kufahamu vema na kuiheshimu Kanuni hii ya Maadili
  • Kuweka malengo halisi ya kazi ili kuwawezesha kufika kiwango cha juu kabisa katika utendaji wao wa kazi.
  • Kuwa wabunifu, wavumbuzi na siku zote kujibidisha kuongeza viwango vya utendaji kwa kujiongezea maarifa na ujuzi
  • Kutumia misingi ya haki, badala ya upendeleo, katika utoaji wa huduma.
  • Kuwa msafi wa kuvaa nguo za heshima zinazokubalika mahali pa kazi
  • kujitahidi kudumisha uhusiano mzuri mahali pa kazi na utendaji wa pamoja kwa:-
  • Kutoa maelekezo ambayo ni wazi, sahihi na ya kueleweka;
  • Kuepuka kufanya vitendo viovu au kutamka maeneno yanayolenga kuwaaibisha Watumishi wa ngazi moja, za chini yao au wa vyeo vya juu;
  • Kuepuka matumizi ya lugha mbaya matusi, Utani na hasira katika utendaji wa kazi;
  • Utafakari ipasavyo maoni rasmi yanayotolewa na Watumishi wengine na hata walio chini yao;
  • Kufanya Mikutano ya Watumishi mara kwa mara ;
  • Kuhakikisha kwamba Watumishi walio chini yao wanaweka malengo halisi ya kazi, kufuatilia utendaji wao mara kwa mara na kuwahimiza kuongeza uwezo na ujuzi wao katika utendaji;
  • Kutoa Taarifa za tathmini ya utendaji kwa Watumishi bila upendeleo.
  • Kutoa sifa au tuzo kwa Watumishi wenye utendaji bora na
  • Kuwaheshimu Watumishi Wenzao pamoja na kuheshimu kazi zao, hasa haki za faragha wanaposhugulikia taarifa zao za siri na binafsi.

Utii kwa Serikali

  • Watumishi  wa Umma wanapaswa kutii Serikali iliyopo madarakani
  • Kwa hiyo, Watumishi wa Umma wanatakiwa kutekeleza sera na maelekezo halali yanayotolewa na Mawaziri na Viongozi wao wengine wa Serikali.

 

Bidii ya Kazi

Watumishi wa umma wanapaswa kufanya kazi kwa bidii na nidhamu ya hali ya juu. Vilevile wanapaswa kuonyesha kwamba wanaheshimu na kujali wajibu wao kwa kufanya yafuatayo:-

  • Kutumia maarifa, ujuzi na utaalam wao ili kupata ufanisi wa kiwango cha juu na kuzikamilisha katika muda unaotakiwa
  • kuepuka mwenendo mbaya ambao utaathiri ufanisi katika utendaji kazi;
  • Kuwa tayari kufanya kazi katika kituo chochote cha kzi atakachopangiwa na
  • Kufika sehemu ya kazi kwa muda uliopangwa na kuzingatia muda rasmi wa kufanya kazi.

Kutoa huduma bila Upendeleo

  • Watumishi wa Umma wanayo haki ya kidemokrasia ya kuwa Wanachama wa Chama chochote cha Siasa. Vile vile wanayo haki ya kuvipigia kura vyama vyao pamoja na viongozi wao wakati wa Uchaguzi Mkuu.
  • Watumishi wa Umma wanapaswa kuzingatia masharti yaliyowekwa katika ushiriki wao katika masuala ya Siasa:-
  • Hawaruhusiwi kufanya wala kujihusisha na masuala ya siasa wakati wa saa za kazi au mahali pa kazi.
  • Kutoa huduma kwa upendeleo kutokana na msimamo wao wa kisiasa; na
  • Kutumia taarifa au nyaraka za kiofisi wanazopata kutokana na utumishi wao kwa Umma kwa manufaa ya vyama vyao.
  • Watumishi wa umma wanayo haki ya kuwasiliana na viongozi au wawakilishi wao wa kisiasa ilimradi wanazingatia yafuatayo:-
  • Waepuke kutumia ushawishi wa kisiasa kuingilia mgogoro wa kikazi baina yao na Serikali.
  • Waepuke kutumia ushawishi wa kisiasa kwa manufaa yao binafsi ambayo sio sehemu ya sera za Serikali.
  • Watumishi wa Umma wanayo haki ya kuabudu na kushiriki dini yoyote wanayoipenda ilimradi kwa kufanya hivyo hawavunji sheria zilizopo. Hata hivyo kwa kuwa Serikali haina dini hairuhusiwi kuhubiri imani za dini wkati wa kazi na mahali pa kazi

Kufanya kazi kwa Uadilifu

  • Watumishi wa Umma wanapaswa kutumia madaraka yaliyokabidhiwa kwa kuzingatia mipaka ya madaraka yao na hawapaswi kutumia madaraka yao kwa manufaa yao binafsi, kuwapendelea marafiki na jamaa zao au kuwakandamiza wengine.
  • Watumishi wa Umma wanapaswa kusimamia vizuri fedha na mali ya Umma waliyokabidhiwa na ni wajibu wao kuzuia uharibufu, upotevu au ubadhirifu usiotoke kutokana na uzembe au manufaa ya mtu binafsi au kandi fulani
  • Watumishi wa Umma wanapaswa kutumia rasilimali za umma kwa manufaa ya Umma. Rasilimali za umma ni pamoja na Mitambo, Vifaa vya Ofisi, Simu, Kompyut, mashine za kunakili mitambo, mashine za kunakili kwa picha, huduma za Umma kama vile umeme, Maji, usafiri nk. majengo na vifaa vinginevyo vilivyonunuliwa kwa fedha za Serikali au kutolewa Msaada kwa Serikali. (Gharama anazorejeshewa Mtumishi  na Serikali au gharama za huduma za nyumbani kwa baadhi ya Watumishi kama vile; Simu maji Umeme huhesabiwa kama ni sehemu ya mali ya umma).
  • Watumishi wa Umma wanapaswa kuwa waaminifu na kutumia muda wa kazi kutekeleza wajibu wao. Hawaruhusiwi kutumia mufa wa kazi kwa shughuli binafsi au kwa mapumziko isipokuwa kama wamepewa idhini ya kufanya hivyo.
  • Watumishi wa Umma hawaruhusiwi kuwaomba au kuwaagiza watumishi walio chini yao kuwafanyia kazi zao binafsi ambao hazina uhusiano na kazi zao za Utumishi wa Umma.
  • Watumishi wa Umma wanatakiwa,  kwa utaratibu ulipwekwa kuwa tayari kutangaza kwa waajiri wao au mamlaka yoyote halali mali walizonaz, za waume au wake zao na mali za ndugu wanaowategemea endapo watatakiwa kufanya hivyo.
  • Watumishi wa Umma wanapaswa kuepuka tabia ambayo inavunja heshima ya Utumishi wao kwa umma hata wanapokuw nje ya mahali pa kazi. Tabia inayowezakuvunja heshima ya Utumishi wa Umma ni pamoja na matumizi ya  madawa ya kulevya, Ulevi kukopa kwa kiwango ambacho hawawezi kurejesha, mwenendo mbaya na kujihusisha na Vitendo vyovyote viovu mbele ya jamii
  • Watumishi wa Umma wanapaswa  kuepuka kutoa zawadi zisizo halali, kuomba kulazimisha au kupokea rushwa ktoka kwa matu yeyeote ambaye waliwahi kumhudumia, wanayemhudumia au wanayetarajia kumhudumia ama kwa kufanya hivyo wao wenyewe au kwa kutumia mtu mwingine.
  • Kwa mujibu wa Kanuni hii Rushwa ni Mapato yasiyo halali ambayo yamepatikana kutokana na matumizi mabaya ya ofisi au madaraka aliyokabidhiwa mtumishi.
  • Watumishi wa Umma au Familia zao wanapaswa kuepuka kuomba, kupokea au kutoa zawadi ambazo zitaonekana kwamba zinalenga kuathiri uadilifu wao.
  • Watumishi wa umma wanapaswa kuepuka kutoa zawadi kwa watumishi wenzao
  • Kwa mujibu wa Kanuni hii, vitu vifuatavyo havihesabiwi kama zawadi  yenye mwelekeo wa rushwa:-
  • Vitu vidogo vidogo vyeye dhamani ambayo vimetengenezwa mahususi kwa kutolewa kama zawadi. Vitu hivyo ni Pamoja na kadi za Salamu, Kikombe cha Washindi wa mashindano mbalimbali Kalenda, Vitabu vya kumbukubu za kila siku (shashara, kalamu nk
  • Kitu chachote ambacho mtumishi wa Umma analipia au kufanya marejesho kulingana na thamana yake;
  • Zawadi yoyote ambayo haipo kwenye maelezo yaliyotangulia hapo juu, inapaswa kukabidhiwa kwa mwajiri na Mtumishi aliyepokea kwa maandishi. Mwajiri anapaswa kukiri kupoklea kwa Maandishi. Mwakuri anapaswa kupokea zawadi kutoka kwa Mtumishi na kuingiza katika rejesta ya zawadi zilizokabidhiwa kwake.
  • Watumishi wa Umma wanapaswa kutumia Sheria,Kanuni na Taratibu zilizopo katika kutekeleza wajibu wao na wakati huo huo kutambua kasoro ambazo zinahitaji marekebisho.
  • Watumishi wa Umma waepuke kuwa na Mahusiano yoyote ya kimapenzi mahali pa kazi na wakati wa kazi. Vilevile, wanapaswa kuepuka tabia yoyote ya unyanyasaji wa kijinsia Matendo ya unyayasaji wa kijinsia ni pamoja na :-
  • Kulazimisha mahusiano ya kimapenzi au upendeleo wa kimapenzi na mtu yoyote,
  • Vitendo vya kubaka , kunajisi na shambulio lolote la aibu,
  • Vitendo vya makusudi ambavyo havikubaliki kama vile kugusana, kufinyana kupapasana, kusuguana au kushikana kwa nguvu sehemu yoyote ya Mwili, nywele au hata nguo;
  • Kutoa masengenyo, ishara, sauti fulani fulani, utani matamshi yoyote yanayolenga jinsia au kiungo chochote cha mwili wa mtu,
  • Kusaidia au kupokea upendeleo , ahadi au zawasdi kutokana na kukubali kuwa na uhusiano wa kimapenzi
  • Kuangalia kuonyesha au kugawa vitu kama vile Picha, filamu, machapisho katika vijarida ambayo huonyesha matukio au vitendo bayana vya mahusiano ya kimapenzi au ambavyo huvunja maadili mema sehemu ya kazi au wakati wa kazi.
  • 5 Watumishi wa Umma ambao wanaombwa na viongozi wao wa kazi kuvunja Sheria au kanuni za Maadili ya utendaji katika Utumishi wa Umma au kanuni za maadili ya kazi za kitaalamu wanapaswa kutoa taarifa kwa kutumia taratibu za serikali zilizopo nza kushughulikia malalamiko. Iwapo Mtumishi ataona malalamiko yanaweza yakaelekezwa moja kwa moja kwa Katibu Mku, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma ambaye atashughulikia malala miko hayo ipasavyo.

 Matumizi sahihi ya Taarifa

  • Watumishi wa Umma hawaruhusiwi kutoa kwa watu wasiohusika taarifa za Serikali, ama za siri au za kawaida ambazo wamezipokea kutoka kwa watu wengine kwa kuamini tu lakini bila idhini. Kwa kuzingatia utunzaji wa siri za serikali, Watumishi hawaruhusiwi pia kutoa taarifa za Serikali kwa Watu wasiohusika hata baada ya kuacha kazi katika Utumishi wa Umma.
  • Watumishi wa Umma hawaruhusiwi kupotosha au kuzuia utekelezaji wa sera na mipango0 ya Serikali kwa kutoa taarifa kwa watu bila idhini kabla sera na mipango hiyo kutangawa rasmi kwa Umma
  • Watumishi wa Ummma hawaruhusiwi kutumia nyaraka au taarifa za Serikali wanazozipata katika kutekeleza wajibu wao kwa manufaa yao binafsi
  • Taarifa za Serikali zitatolewa kwa vyombo vya habari na maafisa wenye madaraka ya kufanya hivyo kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa.
  • Watumishi wa Umma watatoa taarifa za Serikali wanazotaka zipelekwe kwenye vyombo vya habari kupitia kwa maofisa wao wa habari, mawasiliano na elimu au kupitia kwa wakuu wao wa kazi.

Matangazo

  • RATIBA YA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA 2025 April 15, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 04, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • MATOKEO YA DARASA LA NNE 2024 January 04, 2025
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONGORO AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO, ARIDHISHWA NA KASI YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA UMEME

    May 05, 2025
  • JAMII YAASWA KUJENGA UTAMADUNI WA KUWAHUDUMIA WAZEE

    March 19, 2025
  • KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA TAMISEMI YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI MKOA WA RUKWA

    January 09, 2025
  • RAIS SAMIA ATOA ZAWADI ZA MSIMU WA SIKUKUU WA MWAKA MPYA KWA WATOTO YATIMA NA WENYE MAHITAJI MAALUM MKOANI RUKWA

    December 31, 2024
  • Angalia Zote

Video

LIVE- WAZIRI MCHENGERWA ANATAO TANGAZO LA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Miundombinu ya Rukwa
  • Uvuvi
  • Mikakati ya Mkoa
  • Industries
  • Madini
  • Speeches
  • Huduma za Kilimo
  • Regional History
  • Hotuba

Viunganishi Linganifu

  • Pakua Salaryslip yako hapa
  • Idara ya Takwimu (NBS)
  • Mfumo wa Kutuma, Kupokea na kufuatilia Malalamiko, Mapendekezo, Maulizo na Pongezi
  • Watumishi portal
  • Tafuta ajira Serikalini
  • Pata kila kitu kutoka serikalini

World visitors tracker

world map hits counter

Wapitiaji

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa