Kilimo cha zao la kahawa
Mkoa unaendelea na juhudi za kufufua zao la kahawa kwa kuweka msukumo katika usimamizi ili zao hili liweze kuwa moja ya zao la biashara katika Mkoa wetu. Juhudi hizi ni pamoja na kuhamasisha wakulima, kutambua maeneo ya kilimo, kuwapatia mafunzo wakulima na wataalam na kuzalisha miche.
Eneo litakalolimwa zao la kahawa
Baada ya kuhamasisha wakulima, makampuni na taasisi, eneo la kiasi cha ekari 3,195.83 kimebainika kuwa kitafaa kulimwa zao la kahawa. Jumla ya wakulima 2,266 na taasisi 9 zitajihusisha katika uzalishaji wa kahawa.
Kazi zilizofanyika
Ili kuhakikisha juhudi za kufufua zao hili zinafanikiwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ilizielekeza Halmashauri kwenye kikao cha tarehe 10 Januari, 2018 kuanza jitihada za kufufua na jitihadi zilizofanyika ni kama ifuatavyo;
Kilimo cha zao la alizeti.
Mkoa umejipanga katika kuhamasisha kilimo cha zao la alizeti kama zao la biashara. Hali ya uzalishaji wa zao la alizeti katika mkoa umebaki kuwa ni wastani wa gunia 6.5 za kilo 65 kwa ekari sawa na tani 1.1 kwa hekta. Tija hii ni ndogo sana ukilinganisha na tija iliyofanyiwa utafiti ya gunia 12-16 kwa ekari sawa na Zaidi ya tani 2.00 kwa hekta
Sababu za kuwa na uzalisha mdogo ni pamoja na :-
Mkakati wa mkoa ni kufikia malengo yafuatavyo:-
Mkakati wa kufikia malengo.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa