SEKTA YA MALIASILI
Misitu
Raslimali ya Misitu ni muhimu sana katika ustawi wa maisha ya wananchi wa Mkoa Rukwa kiuchumi na kijamii. Misitu husaidia katika upatikanaji wa mvua, hupunguza hewa ya ukaa kwenye mazingira yetu, hutunza vyanzo vya maji, Pia Misitu ni muhimu sana katika shughuli zetu za kiuchumi na za kijamii za kila siku kupitia mazao yake ya mbao, kuni na mkaa.
Mkoa una eneo la hekta 147,917.65 ambazo zimefunikwa na misitu ya asili na ile ya kupandwa. Katika Kipindi cha mwaka 2017/2018 Mkoa umeendelea kuhifadi misitu hiyo kwa mujibu wa sheria na kanuni za uhifadhi zilizowekwa.
Katika kipindi cha mwaka 2017/2018, halmashauri zilijiwekewa malengo ya kupanda jumla ya miti 6,000,000 ili kutekeleza lengo la Kitaifa la kupanda miti 1,500,000 kwa kila Halmashauri. Hadi tarehe 30 Juni, 2018 Mkoa ulipokea taarifa za kupandwa miti 4,686,169 sawa na asilimia 78.1 ya malengo. Miti hii imepandwa katika maeneo mbalimbali.
Jedwali Na 8:Takwamu za upandaji miti kwa mwaka 2017/2018
Halmashauri
|
LENGO
|
Idadi iliyopandwa
|
Asilimia
|
Sumbawanga MC
|
1,500,000 |
935,321 |
62.35 |
Sumbawanga DC
|
1,500,000 |
1,423,448 |
94.5 |
Nkasi DC
|
1,500,000 |
1,320,000 |
83.0 |
Kalambo DC
|
1,500,000 |
1,007,400 |
67.2 |
Jumla
|
6,000,000 |
4,686,169 |
78.1 |
Usimamizi wa Mapori ya Akiba
Mkoa una mapori ya Akiba mawili, ambayo ni Pori la Akiba la Lwafi lenye ukubwa wa kilomita za mraba 2,837.5 na Pori la Akiba la Uwanda lenye ukubwa wa kilomita za mraba 5,000 na kufanya mapori yote mawili kuwa na jumla ya kilomita za mraba 7,837.5.
Mapori haya yamekuwa yakikumbana na changamoto mbalimbali ikiwemo kufanyika kwa shughuli za kibinadamu ndani ya mapori kama vile kuingiza mifugo, kilimo cha mazao, kupasua mbao, kukata miti, kuchoma mkaa, uwindaji haramu na uvuvi usio endelevu.
Katika kipindi cha mwaka 2017/2018 jumla ya doria 24 zimefanyika katika Pori la Akiba la Uwanda na kufanikiwa kukamata majangili 179, ngo’mbe 2,247 na kondoo 141 ndani ya hifadhi na kufanikwa kuendesha kesi 15 za mifugo, kesi 38 za uvamizi wa shughuli za kilimo na uvuvi na kesi 2 za silaha. Jumla ya kesi hamsini na tano (55) zilifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Sumbawanga na kati ya kesi hizo kesi ishirini na saba (27) zilihukumiwa.
Doria 30 zimefanyika katika Pori la Akiba la Lwafi na kuwezesha kukamata majangili 28, ng’ombe 400, baiskeli 14, mbao vipande 462, misumeno 9, pikipiki 2, meno ya tembo 4, malori 2 , mkaa gunia 6, bunduki 2, gobole 7, risasi za shotgun 20 na mtego wa roda 1.
Uwekaji wa Alama au Mabango
Katika kipindi cha 2016/2017 na 2017/2018 jumla ya alama/vigingi 237 vimeshawekwa katika maeneo mbali mbali ya misitu na Mapori ya Akiba kwa mchanganuo ufuatao; Msitu wa Hifadhi ya Mbizi vigingi 22, Msitu wa Hifadhi wa Kalambo vigingi 63, Pori la Akiba la Uwanda vigingi 75 na Pori la Akiba la Lwafi vigingi 77.
Zoezi hili bado halijafanyika katika maeneo yenye changamoto za migogoro ya mipaka baina ya maeneo ya hifadhi na Maeneo ya Vijiji. Alama zilizobaki zitawekwa baada ya kupitia ramani upya na kutatua migogoro iliyopo baina ya Vijiji na maeneo ya Hifadhi hizo.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa