USHIRIKA
Lengo kuu la vyama vya ushirika ni kuunda vyombo vya kiuchumi ambavyo vinaanzishwa na kusimamiwa na wanachama wenyewe.
Huduma zinazotolewa na vyama vya ushirika kwa wanachama ni:-
Mkoa wa Rukwa una jumla ya Vyama vya ushirika 187 kati ya hivyo 118 ni Vyama vya Akiba na Mikopo (SACCOS), Vyama vya mazao (AMCOS) hamsini na nne (54), Vyama vya Uvuvi vinne (4) naVyama vya wafugaji sita ngombe (6). Chama cha wafugaji nyuki kimoja (1) vyama vya wauza bidhaa/huduma vinne (4) na chama cha ufundi kimoja (1)
Jumla ya wanachama ni 18,908 (wanaume 12,041 wanawake 6,727 vikundi 138 na taasisi 2). Jumla ya thamani ya hisa za wanachama ni Shilingi 893,824,000.00 Akiba ni Shilingi 2,262,538,000.00 na Amana zenye thamani ya Shilingi 3,643,000.00 Jumla ya mikopo yenye thamani ya Shilingi 11,262,268,000 imetolewa na kiasi cha Shilingi 9,330,198,000.00 kimerejeshwa sawa na asilimia 82 ya fedha zilizokopeshwa.
MCHAKATO WA UANZISHAJI WA CHAMA KIKUU.
Kwa Mujibu wa sharia ya vyama vya Ushirika Na. 6 ya mwaka 2013kifungu cha 29 (2) kinaelekeza ili chama kikuu kiweze kuandikishwa kinahitajika kuwa na wanachama wasiopungua ishirini ambao ni vyama vya msingi.
Hadi kufikia Juni 2018 Mkoa una vyama 54 na vyama hivi vimeandikishwa kati ya 2014 na 2018 hivyo bado ni vichanga na vinajengewa uwezo wa kiuchumi.
Katika kuanzisha chama kikuu jambo kubwa linaloangaliwa ni uwezo wa kiuchumi wa vyama wanachama .Azimio la kuanzisha chama kikuu cha wakulima limetolewa katika Jukwaa la vyama vya Ushirika lililofanyika tarehe 1 Juni 2018 , Kazi ya kuhamasisha vyama vya wakulima kuunda chama kikuu imeanza.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa