SEKTA YA UVUVI
Sekta ya uvuvi ina mchango mkubwa kwa wananchi wa Mkoa wa Rukwa katika kuwapatia lishe bora, ajira na kipato kwa mwananchi mmoja mmoja na hivyo kuchangia kuondoa umasikini na kukuza pato la Taifa.
Shughuli za uvuvi katika Mkoa hufanyika katika Maziwa mawili makubwa ambayo ni Ziwa Tanganyika na Ziwa Rukwa na kwa kiasi kidogo katika mabwawa mawili ya asili ambayo ni Kwela (Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga) na Sundu (Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo). Kadhalika shughuli hizi za Uvuvi hufanyika katika mito na mabwawa yanayochimbwa na wananchi katika maeneo mbalimbali ya Mkoa.
Katika kipindi cha mwaka 2017/2018 jumla ya tani 2,008 za samaki zenye thamani ya shilingi bilioni 9.8 zilivunwa na kusafirishwa ndani na nje ya Mkoa wetu. Fedha hizi ni mapato ya wavuvi wetu kwenye masoko mbalimbali.
Mikakati ya kuendeleza sekta ya Uvuvi
Ili kukabiliana na Changamoto za sekta ya Uvuvi Mkoa unaendelea kushauri na kuhimiza Halmashauri kutekeleza mikakati ifuatayo:
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa