VIWANDA
Idadi ya Viwanda vilivyopo kaatika Mkoa
Kwa mujibu wa orodha ya viwanda iliyopokelewa kutoka katika Halmashauri zote ,Mkoa una jumla ya viwanda 901,(viwanda vidogo sana 809, viwanda vidogo 85, viwanda vya kati 3 na viwanda vikubwa 4.)
Utekelezaji wa kampeni ya “Mkoa wetu, Viwanda Vyetu”.
Katika kutekeleza azma ya Serikali ya awamu ya tano ya kujenga uchumi wa viwanda unaojielekeza katika kufikia Malengo ya Dira ya Maendeleo ya taifa kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025, Serikali ilizindua Kampeni ya “ Mkoa Wetu, Viwanda Vyetu” mwezi Novemba 2017. Kampeni hii inalenga ujenzi wa viwanda vikubwa vya kati na vidogo ili kufikia lengo la kila Mkoa kujenga viwanda visivyopungua 100 ifikapo Desemba ,2018.Mkoa umeanza utekelezaji wa kampeni hiyo ambapo hadi kufikia june 30, 2018 jumla ya viwanda vipya vilivyojengwa ni 54. Takwimu za viwanda hivyo kwa kila Halmashauri ni kama ifuatavyo;
Idadi ya viwanda vilivyoanzishwa.
Halmashauri
|
Lengo
|
Idadi Ya Viwanda Vipya Vilivyojengwa Kufikia Juni 30,2018
|
|||
Vikubwa
|
Kati
|
Vidogo
|
Viwanda Vidogo Sana
|
||
Sumbawanga MC
|
25 |
0 |
1 |
13 |
0 |
Sumbawanga DC
|
25 |
0 |
0 |
0 |
19 |
Nkasi DC
|
25 |
1 |
0 |
11 |
0 |
Kalambo DC
|
25 |
0 |
0 |
11 |
0 |
Jumla
|
100 |
1 |
1 |
35 |
19 |
Maeneo Yaliyotengwa Kwa Ajili Ya Viwanda
Halmashauri zimetenga Jumla ya hekta 1154.48 kwa ajili ya uwekezaji wa Viwanda katika maeneo mbalimbali. Changamoto kubwa katika maeneo haya ni kutokuwepo kwa Miundo mbinu kama Maji, umeme na barabara pia kutolipwa kwa fidia kwa baadhi wadau waliokuwa wakiyamiliki maeneo hayo hapo awali.
Timu Ya Kuendeleza Viwanda Katika Mkoa
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa aliunda timu maalum itakayofanya kazi ya kuratibu maendeleo ya viwanda katika Mkoa inayojumuisha wadau kutoka sekta ya Umma na sekta Binafsi ili kufanya jitihada za pamoja katika kutekeleza azma ya ujenzi wa viwanda katika Mkoa wetu kwa ufanisi kwa kufanya mambo yafuatayo;
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa