Seksheni hii ina lengo la kusaidia au kuwezesha utoaji huduma za uendelezaji wa Elimu ikijumuisha usimamizi wa elimu ya awali, msingi, sekondari, elimu ya watu wazima na inayotolewa katika njia isiyo rasmi; na mitihani ya shule za msingi, sekondari na vyuo vya ualimu. Seksheni hii inaongozwa na Katibu Tawala Msaidizi ambaye pia ni Afisa Elimu wa Mkoa ambaye anawajibika kwa Katibu Tawala wa Mkoa.
Majukumu ya Seksheni ya Huduma za Elimu
ELIMU YA AWALI
Idadi ya Shule zenye madarasa ya Elimu ya Awali ni 367 (Serikali 358 na zisizo za Serikali 9). Shule ya msingi ya wanafunzi wenye mahitaji maalum ya Malangali katika Manispaa ya Sumbawanga ndio inayokosa darasa la Elimu ya Awali.
Idadi ya wanafunzi Elimu ya Awali waliotarajiwa kuandikishwa ni 37,622 (wavulana 18,642 wasichana 18,980). Idadi ya walioandikishwa ni 43,065 (wavulana 21,108 wasichana 21,957) sawa na asilimia 112. Hivyo kuna ongezeko la wanafunzi 5,443.
ELIMU YA MSINGI
Idadi ya Shule za msingi ni 368 (Serikali 359 na zisizo za serikali 9).
Idadi ya wanafunzi waliotarajiwa kuandikishwa darasa la kwanza ni 49,518 (wavulana 24,587 wasichana 24,931). Idadi ya walioandikishwa ni 71,582 (wavulana 35,323 na wasichana 36,259) sawa na asilimia 144. Kuna ongezeko la wanafunzi 22,064.
Idadi ya wanafunzi katika shule za msingi darasa la I-VII ni 252,355 (Wavulana ni 123,537 wasichana 128,818).
Mahitaji ya walimu ni 6508 wakati waliopo ni 4189 na upungufu ni 2319 sawa na 36%.
ELIMU YA SEKONDARI
Mkoa wa Rukwa una idadi ya shule za Sekondari zipatazo 90 kati ya hizo shule za Serikali zikiwa 69 na zisizo za serikali 21. Kati ya shule 90 za Sekondari zilizopo Shule 13 zina kidato cha 5 na 6 (Serikali 10 na zisizo za Serikali 3). Aidha shule 3 za Serikali zimepata Kidato cha 5 kwa mwaka 2017 ambazo ni; Kipeta, Mpui na Vuma zilizoko katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. Shule hizi zimepangiwa wanafunzi wa kidato cha tano kama ifuatavyo; Kipeta wavulana 36, Vuma wavulana 68 na Mpui wasichana 36.
Idadi ya wanafunzi kwa shule za Sekondari za Serikali ni 27939 (wav 14,942 na was 12,997)
Mahitaji ya walimu ni 1724, waliopo ni 1511 upungufu ukiwa walimu 213. Upungufu huu ni kwa walimu wa Sayansi tu. Aidha, Mkoa ulipangiwa walimu wapya 91 wa masomo ya Sayansi, Hisabati na Wataalam wa Maabara 10. Walioripoti ni walimu 80 na Wataalam wa Maabara 6.
ELIMU MAALUMU
Mkoa una shule moja ya Elimu Maalumu ambayo ni shule ya msingi Malangali iliyopo Manispaa ya Sumbawanga. Aidha kuna Vitengo 14 kama inavyojionesha kwenye jedwali
Halmashauri |
S/n |
Kitengo |
Aina ya Ulemavu |
Idadi ya wanafunzi |
||
Wav |
Was |
Jml |
||||
Kalambo
|
1 |
Mbuluma
|
Viziwi
|
3 |
0 |
3 |
Mtindio wa Ubongo
|
1 |
1 |
2 |
|||
Viungo
|
1 |
0 |
1 |
|||
2 |
Kilesha
|
Mtindio wa ubongo
|
3 |
2 |
5 |
|
Uoni hafifu
|
2 |
2 |
4 |
|||
3 |
Kipwa
|
Mtindio wa ubongo
|
5 |
3 |
8 |
|
Bubu
|
2 |
0 |
2 |
|||
Viungo
|
3 |
2 |
5 |
|||
4 |
Myunga
|
Mtindio wa ubongo
|
5 |
2 |
7 |
|
Uoni hafifu
|
3 |
1 |
4 |
|||
Viungo
|
3 |
2 |
5 |
|||
Viziwi
|
2 |
0 |
2 |
|||
5 |
Matai ‘A’
|
Bubu
|
2 |
1 |
3 |
|
Mtindio wa ubongo
|
2 |
2 |
4 |
|||
Usonji
|
0 |
1 |
1 |
|||
Viungo
|
0 |
1 |
1 |
|||
6 |
Msanzi ‘A’
|
Mtindio wa ubongo
|
3 |
2 |
5 |
|
Bubu
|
0 |
1 |
1 |
|||
Viungo
|
1 |
0 |
1 |
|||
Nkasi
|
7 |
Isunta
|
Ulemavu wa akili
|
14 |
8 |
22 |
Viziwi
|
3 |
1 |
4 |
|||
8 |
Machete
|
Ulemavu wa akili
|
6 |
4 |
10 |
|
9 |
Kirando
|
Ulemavu wa akili
|
3 |
6 |
9 |
|
Viziwi
|
2 |
1 |
3 |
|||
Uoni hafifu
|
0 |
1 |
1 |
|||
Ulemavu wa viungo
|
3 |
2 |
5 |
|||
Sumbawnga (M)
|
10 |
kizwite
|
Viziwi
|
17 |
11 |
28 |
Ulemavu wa akili
|
11 |
3 |
14 |
|||
Ulemavu wa ngozi
|
21 |
21 |
42 |
|||
Uoni hafifu
|
10 |
12 |
22 |
|||
Wasioona
|
10 |
17 |
27 |
|||
11 |
Katandala
|
Ulemavu wa akili
|
4 |
3 |
7 |
|
12 |
Mwenge
|
Ulemavu wa akili
|
5 |
8 |
13 |
|
Sumbawanga (V)
|
13 |
Laela ‘A’
|
Ulemavu wa akili
|
6 |
4 |
10 |
14 |
Mukamanye
|
Ulemavu wa akili
|
2 |
2 |
4 |
|
Viziwi
|
1 |
3 |
4 |
|||
JUMLA |
159 |
130 |
289 |
ELIMU YA UALIMU:
Mkoa una jumla ya Vyuo vya Ualimu vinne (4) ambapo Vyuo vitatu (3) vinamilikiwa na Taasisi zisizo za Serikali ambavyo ni; Chuo cha Ualimu Aggrey, Rukwa na St. Maurus na Chuo kimoja (1) cha Ualimu cha Serikali ambacho ni Sumbawanga.
VYUO VYA UFUNDI STADI
Mkoa unavyo Vyuo vya Ufundi Stadi vipatavyo 4, kama inavyooneshwa katika jedwali.
|
|
|
|
|
|
||
|
|
|
|
|
|||
2.
|
|
|
|
3.
|
|
|
|
ELIMU YA CHUO KIKUU
Mkoa una kituo 1 cha chuo kikuu Huria na Chuo kikuu cha Sayansi Tawi la Mbeya (Mbeya Universty of Sience and Technology- MUST) kilichopo katika eneo lililokuwa kambi ya ujenzi la Kianda katika Halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga. Hadi sasa Chuo kikuu cha MUST kimeshakabidhiwa eneo hilo pamoja na majengo yaliyokuwa kwenye kambi hilo kwa ajili ya kuanza kazi
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa