Tuesday 21st, January 2025
@
Mkoa wa Rukwa utaendesha kampeni ya utoaji chanjo ya Polio kwa awamu ya nne kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano kote katika wilaya tatu za Nkasi, Kalambo na Sumbawanga.
Kampeni hiyo itazinduliwa tarehe 01 Desemba 2022 katika kijiji cha Kirando wilaya ya Nkasi ambapo mgeni rasmi atakuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Queen Sendiga.
Wananchi wa maeneo jirani na Kirando mnaalikwa kujitokeza kwenye kampeni hiyo pia wito unatolewa kwa wazazi na walezi wenye watoto wenye umri lengwa yaani chini ya miaka mitano kutoa ushirikiano kwa wataalam wa afya watakapopita kwenye kwenye maeneo yao kutoa chanjo hiyo kuanzia tarehe 01 hadi 04 Desemba 2022.
Mwisho
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa