Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi
Hali ya uvuvi Mkoani
Mkoa una idadi ya wananchi 14,094 wanaojishughulisha moja kwa moja na uvuvi na wananchi 1,021 wanaojishughulisha na uchakataji wa mazao ya uvuvi. Wavuvi wanamiliki mitumbwi ya uvuvi 2,820. Katika Mkoa, shughuli za uvuvi zinafanyika kwa kiasi kikubwa katika maziwa mawili makubwa ambayo ni Ziwa Tanganyika na Rukwa na kwa kiasi kidogo katika maziwa madogo mawili ya asili ambayo ni Kwela na Sundu. Halikadhalika Uvuvi hufanyika katika mito 87 na mabwawa 481 yaliyochimbwa na wananchi katika maeneo mbalimbali ya Mkoa.
Fedha hizi ni mapato yaliyotokana na uvuvi wa samaki katika maeneo mbalimbali ya Mkoa. Kwa mwaka 2022/2023 jumla ya tani 3,178.41 za samaki na tani 162.81 za dagaa zilivuliwa katika mkoa wa Rukwa. Mchanganuo ufuatao umeelezea zaidi
Aina ya zao la uvuvi
|
Gharama za ujazo
|
Julai 2022 hadi Juni, 2023
|
Samaki
|
Tani
|
3,178.41
|
|
Kiasi (shilingi)
|
18,956,463,345.80
|
Dagaa
|
Tani
|
162.81
|
|
Kiasi (shilingi)
|
676,767,871.36
|
Ujenzi wa soko la samaki la Kasanga
Katika kuhakikisha kuwa, huduma katika ukanda wa wavuvi zinaboreshwa, Wizara ya Mifugo na Uvuvi imejenga soko la samaki katika kijiji cha Lusambo kilichopo Kata ya Kasanga katika Wilaya ya Kalambo. Ujenzi huu unafadhiliwa na fedha za UVICO kupitia programu ijulikanayo kama Extended Credit Facilities (ECF). Ujenzi wa soko la samaki Kasanga unasimamiwa na Kampuniya Nice Contractor and Energy Supplies Ltd kwa gharama ya shilingi 1,409,580,965.20 Mwalo wa samaki wa Kirando. Ujenzi wa soko umefikia asilimia 95 ya kazi yote iliyoanza mwezi machi, 2023 na inatarajiwa kukamilika mwezi Novemba, 2023.
Viwanda vya Usindikaji Mazao ya Uvuvi
Katika Mkoa kuna viwanda viwili vya kusindika na kuhifadhi samaki vinavyomilikiwa na sekta binafsi ambavyo ni;-
Tanganyika Fresh Fish Ltd kipo Samazi-Kalambo chenye uwezo wa kugandisha barafu /cold freeze kuanzia tani 3 hadi tani 5 kwa siku,
Kupitia taasisi ya The Nature Conservancy ilivipatia vikundi vya usimamizi wa rasilimali za maji (BMU) kwa kuwapa boti 4 za doria kwa vikundi vya Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi katika Kata nne za Itete, Kipili, Kirando na Mkinga.
Mwanamama Kutoka Kasanga Wilaya ya Kalambo akiwa ameshika Samaki wa Ziwa Tanganyika
Kasanga, Wilayani Kalambo, Ziwa Tanganyika
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa