Kwa mujibu wa Kifungu cha 9 (1) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya Mwaka 2024, ili mtu aweze kuandikishwa kuwa Mpiga Kura anatakiwa kuwa sifa zifuatazo:
(i) Awe Raia wa Tanzania;
(ii) Awe ametimiza umri wa miaka 18 ; na
(iii) Awe hajapoteza sifa kwa mujibu wa Sheria za Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya Mwaka 2024 au Sheria nyingine yoyote iliyotungwa na Bunge..
Baada ya kutimiza sifa hizi, mtu unatakiwa kufuata utaratibu ufuatao:
1. Utaenda kituo cha kuandikisha Wapiga Kura kilichopo jirani na maeneo unayoishi.
2. Utajitambulisha kwa Mwandishi Msaidizi na Mwandishi Msaidizi atakuuliza maswali na atakujazia fomu maalum
3. Utaenda kwa BVR kit Operator kwa ajili ya kuchukuliwa alama za kielektroniki ikiwa ni pamoja na kupigwa picha
4. Utapewa kadi ya Mpiga Kura na unatakiwa uihakiki majina yako, picha na taarifa nyingine, kama kipo sahihi na baada ya kujiridhisha utaondoka kituoni.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa