Sekta ya Viwanda na biashara ni muhimu sana katika Mkoa wetu kwani inasaidia katika kuongeza ajira kwa wananchi na kukuza uchumi wa Mkoa na nchi kwa ujumla. Katika sekta hii kuna viwanda vidogo na vya kati vinavyoendeshwa. Viwanda hivyo vinahusisha shughuli za usindikaji wa nafaka, samaki, nyama na kiwanda cha kutengeneza sabuni.
Kwa upande wa biashara, Mkoa umekuwa ukijitahidi katika kuhakikisha kuwa inawakwamua wananchi wake kiuchumi. Katika jitihada hizo maafisa biashara wamekuwa wakitoa elimu na ushauri kwa wajasiriamali juu ya kuendesha biashara zao kwa mafanikio na uboreshaji wa vifungashio kwa wasindikaji ili kuwavutia wateja na
kuongeza mauzo. Pia wamekuwa wakitoa elimu juu ya umuhimu wa ulipaji wa kodi kwa wakati na kuwapa na leseni za biashara.
Sekta ya Viwanda na biashara ni muhimu katika kuongeza ajira kwa wananchi na kukuza uchumi wa Mkoa. Viwanda vilivyopo katika mkoa ni viwanda vidogo sana na vya kati vinavyoendeshwa na sekta binafsi. Viwanda hivyo vinashughulika na usindikaji wa nafaka, samaki, nyama na maji. Mkoa una maeneo mengi yanayofaa kwa uwekezaji wa viwanda hasa katika maeneo yafuatayo:-
Jumla ya hekta 809. Zimeanishwa katika Halmashauri kwa ajili ya kuvutia sekta binafsi kujenga viwanda vya aina mbalimbali
Idadi ya viwanda vilivyopo katika mkoa
Kwa mujibu wa orodha ya viwanda Tanzania Bara kwa takwimu za Desemba 2015 - Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Mkoa wa Rukwa una takribani viwanda 950 (viwanda vidogo sana 869, ni viwanda vidogo 78,Viwanda vya kati 2 kiwanda kikubwa 1)
Jedwali Na. -------- idadi ya viwanda vilivyopo katika mkoa kwa kigezo cha ajira.
Aina ya kiwanda
|
Idadi ya waajiriwa
|
Idadi ya viwanda
|
Asilimia
|
Viwanda vidogo sana
|
1 hadi 4
|
869 |
91.50 |
Viwanda vidogo)
|
5 hadi 49
|
78 |
8.2 |
Viwanda vya kati
|
50 hadi 99
|
2 |
0.2 |
Viwanda vikubwa
|
100 na zaidi
|
1 |
0.1 |
JUMLA |
950 |
100.00 |
Mikakati wa mkoa wa kuendeleza viwanda.
Agenda ya Viwanda 100 kila Mkoa - 30 Juni, 2019
Katika kutekeleza Agenda ya uanzishwaji wa viwanda 100 Mkoa umefanikiwa kujenga viwanda vipya 124 kati ya hivyo vidogo sana ni 86, vidogo 36, cha kati 1 na kikubwa 1.
Hadi kufikia 30 Juni, 2019 Mkoa wetu ulikuwa na jumla ya viwanda 1,024 kwa mchanganuo ufuatao:-
Viwanda vikubwa 5,
Viwanda vya kati 4,
Viwanda vidogo 120, na
Viwanda vidogo sana 895
Jedwali Na: 8 Mchanganuo wa viwanda vilivyopo katika Mkoa
Na.
|
Ukubwa wa kiwanda
|
Aina ya kiwanda
|
Idadi
|
||
1
|
Vidogo sana
|
Usindikaji nafaka(mahindi)
|
644
|
||
2
|
Ushonaji nguo
|
228
|
|||
3
|
Ushonaji viatu
|
4
|
|||
4
|
Utengenezaji majiko ya kupikia
|
11
|
|||
5
|
Uhunzi
|
8
|
|||
Jumla ya Viwanda vidogo sana |
895
|
||||
6
|
Vidogo
|
Usindikaji nafaka(mahindi)
|
29
|
||
7
|
Kusindika nafaka(mpunga)
|
24
|
|||
8
|
Ukamuaji Alizeti
|
19
|
|||
9
|
Utengenezaji wa samani
|
12
|
|||
10
|
Uokaji mikate na maandazi
|
5
|
|||
11
|
Usindikaji wa Samaki
|
5
|
|||
12
|
Utengenezaji wa sabuni
|
1
|
|||
13
|
Uchomeleaji
|
25
|
|||
Jumla ya Viwanda vidogo |
120
|
||||
14
|
Vyakati
|
Usindikaji nafaka (mahindi)
|
3
|
||
15
|
Kiwanda cha Gesi
|
1
|
|||
Jumla ya Viwanda vya Kati |
4
|
||||
16
|
Vikubwa
|
Usindikaji nyama
|
1
|
||
17
|
Uzalishaji wa Makaa ya mawe
|
1
|
|||
18
|
Usindikaji nafaka(mahindi)
|
2
|
|||
19
|
Uzalishaji wa maji
|
1
|
|||
Jumla ya Viwanda vikubwa |
5
|
||||
Jumla kuu ya Viwanda Kimkoa
|
1,024
|
Kiwanda cha Maji ya kunywa cha Dew Drop
Kiwanda cha Energy Milling, Sumbawanga.
SAAFI kiwanda cha Nyama
Mpunga ni miongoni mwa Zao Kuu la Kibiashara katika Mkoa wa Rukwa
Viazi Lishe navyo hurahisishwa na kuwa chakula kitamu
Samaki wa Kukaushwa wa Ziwa Rukwa
Asali pia inapatikana kwa Wingi katika Wilaya zote za mkoa wa Rukwa
Mafuta ya Karanga yanapatikana Sumbawanga
Unga wa Mahindi ya njano
Ulezi, Ngano na Unga wa ngano.
Dagaa Kutoka Ziwa Tanganyika, Wilaya za Nkasi na Kalambo
Unga wa Muhogo wa Wilaya ya Nkasi
Samaki aina ya Mikebuka
Mchele safi wa Rukwa
Maharage aina ya Ulambo
Unga wa Dona
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa