Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Sumbawanga
Serikali kupitia mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania imepata mkopo nafuu kiasi cha Shilingi Billion 55.9 kutoka Benki ya Maendeleo ya Ulaya (EUROPEAN INVESTMENT BANK – EIB) kwa ajili ya ujenzi wa kiwanja hiki kwa kiwango cha kimataifa. Na Serikali italipa kiasi cha Tanzania Shilingi Billion 3.3 kwa Wahanga wapatao 97, kutoka Kata zote mbili yaani Kata ya Sumbawanga Asilia wapato 27 na Kata ya Izia 70 na kufikia jumla ya Wahanga 97. Kazi hii itahusisha (Scope) maeneop yafuatayo;
Baada ya ujenzi huu kukamilika utawezesha kiwanja cha ndege cha Sumbawanga kutumika kwa masaa 24 na kipindi chote cha mwaka.
Ziara ya Naibu Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi Mh. Atashasta Nditiye walipopita katikati ya Uwanja wa Ndege wa Sumbawanga
Mpango wa Kujenga Kiwanja cha Ndege Eneo la Kisumba
Mkoa umetenga eneo lenye ukubwa wa Hekari 3,411 katika eneo la Kisumba Manispaa ya Sumbawanga kwa ajili ya ujenzi wa Kiwanja cha Ndege. Eneo hili linamilikiwa na Meneja, Kiwanja cha Ndege Sumbawanga. Matarajio ni kujenga Kiwanja cha Ndege cha kisasa ili kuongeza fursa za usafiri na kuchochea shughuli za kiuchumi. Kwa mujibu wa Meneja wa TANROADS ambaye ana dhamana ya ujenzi na ukarabati wa Viwanja vya Ndege, usanifu (Design) unatarajiwa kuanza Mwaka wa Fedha 2019/2020
Uboreshaji wa bandari zilizopo katika Mkoa wa Rukwa
Bandari ya Kasanga
Bandari ya Kasanga ina Gati la kuegesha Meli lenye urefu wa Mita 20 na kina cha maji cha mita 8-10 kutegemeana na msimu wa mvua pia lina uwezo wa kuhudumia meli moja kwa wakati mmoja. Katika kipindi cha miaka mitatu 2014/2015 – 2016/2017, bandari ilihudumia jumla ya tani 63,310 kati ya hizo tani 57,739 ilikuwa ni shehena ya kwenda nje ya Nchi (Export) na tani 5,571 ilikuwa ni shehena ya kwenda ndani ya Nchi (Inward/ Outward).
Upanuzi wa Bandari ya Kabwe
Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) imeanza kufanya upanuzi wa Bandari ya Kabwe. Upanuzi huo unatarajia kugharimu Shilingi bilioni 7.5. Aidha, Mkandarasi SUMRY ENTERPRISES LTD ameingia Mkataba wa kufanya kazi hiyo kwa muda wa miezi 18 kuanzia tarehe 2 Aprili, 2018. Mamlaka ya Bandari tayari imekwisha lipa fidia kiasi cha Shillingi 160,743,498.00 kwa wananchi 37 waliopisha eneo hilo kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya bandari.
Bandari ya Kipili
Novemba, 2015 – Juni, 2016 Bandari ilipokea shehena ya Tani 1298, Julai, 2016 – Juni, 2017 Bandari ilipokea shehena ya Tani 978, Julai 2017 – Juni, 2018 Bandari ilipokea tani 626. Maeneo yafuatayo yanatakiwa kuboreshwa ili kuongeza ufanisi;
Mawasiliano ya Kidigitali
Mkongo wa Taifa (NICTBB)
Mkoa wa Rukwa unahudumia jumla ya vituo vitatu (3) vya mkongo wa Taifa ambavyo ni Miangalua, Sumbawanga T/House na Kizi.. Aidha Mkoa unahudumia jumla ya km 240 ya mkongo wa Taifa zilizogawanyika kama ifuatavyo:
Wateja wa Mkongo wa Taifa
TTCL inaendelea kuhakikisha kuwa inakuwa ndio muhimili wa teknolojia ya habari na Mawasiliano (Tehama) nchini; na leo TTCL kwa Mkoa wa Rukwa na Katavi imeunganisha wateja mbali mbali kwenye mkongo wa Taifa kama ifuatavyo:-
SUMBAWANGA: TANROAD, TRA, TANESCO, Mahakama ya Mkoa, Benki ya Posta, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Hazina ndogo, Sumatra, Water Reed, Manispaa ya Sumbawanga, Halmashauri ya Sumbawanga, NSSF, NHIF, NMB, CRBD, TPC, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Hospitali ya Rufaa Rukwa, NIC, SUWASA , MUST RUKWA Campus, Chuo Kikuu Huria na Maktaba ya Mkoa.
Shirika la Posta Tanzania
Utekelezaji wa kazi zinazofanywa na Shirika la Posta
Ofisi kuu ya Shirika la Posta Mkoa wa Rukwa ipo barabara kuu mtaa wa Mbeya Road, mkabala na Hospital kuu ya Mkoa wa Rukwa, Sumbawanga.
Huduma zinazotolewa na Shirika la Posta Rukwa
Ujenzi wa barabara
Sumbawanga - Matai kasanga port (km 112)
Kazi ya ujenzi wa barabara bado inaendelea. kwa ujumla kazi imekamilika kwa asilimia 71.6 na kutarajiwa kumalizika 30 Septemba 2018.
Miundombinu ya Barabara
Mkoa wa Rukwa una barabara zenye urefu wa kilometa 1,245.60 zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ambazo zinasimamiwa na Ofisi ya Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Rukwa. Kati ya barabara hizo, kilometa 407.94 ni Barabara Kuu (Trunk Roads) na kilometa 837.66 ni Barabara za Mkoa (Regional Roads). Mchanganuo wa aina na urefu wa barabara hizo ni kama inavyoonyeshwa katika Jedwali Na.10 hapa chini.
Kwa upande wa Miundombinu, Serikali imeendelea kujenga na kukarabati barabara pamoja na Miundombinu mingine. Barabara mpya zilizoanza kujengwa katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Nne zimekamilika. Barabara hizo ni zifuatazo:-
Na |
Jina la Mradi |
Aina ya Mradi |
Gharama (Sh. Milioni) |
Muda wa Utekelezaji (Tarehe) |
Maendeleo na Maelezo Mengine Muhimu |
|
Kuanza |
Kwisha |
|||||
1
|
Sumbawanga – Chala - Kanazi
|
Ujenzi kwa kiwango cha lami
|
78,840.600 |
10.3.2013
|
31.11.2017
|
Kazi imekamilka
|
2
|
Kanazi – Kizi - Kibaoni
|
Ujenzi kwa kiwango cha lami
|
82,841.779 |
10.4.2010
|
31.7.2017
|
Kazi imekamilika
|
3
|
Sumbawanga – Matai – Kasanga Port
|
Ujenzi kwa kiwango cha lami
|
133,286.603 |
13.1.2010
|
11.11.2018
|
Kazi inaendelea
|
4
|
Matai - Kasesya
|
Ujenzi kwa kiwango cha lami
|
|
|
|
Kazi bado kutangazwa
|
5
|
Momba Bridge
|
Ujenzi wa daraja la Momba
|
17,718.145 |
24.7.2014
|
24.7.2019
|
Kazi imekamilika
|
6
|
Sumbawanga Airport
|
Ujenzi kiwango cha lami
|
55,908.850 |
|
|
Fidia imelipwa. Ujenzi bado kuanza
|
TARURA
Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (Tanzania Rural and Urban Roads Agency) kwa kifupi TARURA umeanzishwa rasmi kwa mujibu wa Sheria ya Wakala za Serikali Sura 245 (Executive Agencies CAP 245) na kutangazwa rasmi katika Gazeti la Serikali Na. 211 la tarehe 12/05/2017.
Wakala huu umeanzishwa rasmi tarehe 1/7/2017 kwa ajili ya kutekeleza majukumu ya kiutendaji zaidi kuhusu maendeleo ya barabara za vijijini na mijini. Majukumu hayo ni ya ujenzi, matengenezo pamoja na menejimenti ya barabara za vijijini na mijini.
Mtandao wa Barabara za Mkoa wa Rukwa
Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini kwa Mkoa wa Rukwa unasimamia matengenezo ya barabara zenye urefu wa Km 2,304.18, kati ya lami/zege ni km 34.22,changarawe km 694.09, udongo Kilomita 1,575.87 na vivuko 1,986 vya aina tofauti kama ilivyofafanuliwa hapa chini kwenye Jedwali Na.12 Takwimu hizo ni hadi mwezi Juni, 2019.
Daraja kubwa lenye urefu wa mita 84 Mto Momba
Ujenzi wa daraja la Momba katika eneo la Kilyamatundu/Kamsamba lenye urefu wa meta 84 imekamilka. Kazi ya ujenzi wa daraja inafanywa na Mkandarasi Jiangxi Geo-Engineering (Group) Corporation kutoka China kwa gharama ya Shilingi million 17,718.145. Mkataba wa ujenzi ulisainiwa tarehe 14 Julai, 2017 na kazi ilianza tarehe 1 Agosti, 2017. Kazi ya ujenzi itachukua muda wa miezi kumi na tatu (13) kukamilika ikijumuisha mwezi mmoja wa maandalizi. Kazi ya ujenzi wa daraja ilitarajia kukamilika ifikapo tarehe 31 Agosti 2018. Hata hivyo kazi haikuweza kukamilika kutokana na mto kujaa maji nakupelekea kuongenza muda wa kukamilisha kazi hadi tarehe 24 Julai, 2019. Kazi ya ujenzi imekamilika na daraja linapitika.
Kazi ya Usimamizi inafanywa na TANROADS Engineering Consultancy Unit (TECU) chini ya Meneja wa TANROADS Mkoa wa Rukwa. Gharama ya usimamizi hadi sasa ni Shilingi milioni 353.80625.
Huduma za Kibenki
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa