SEKTA YA MADINI
Umuhimu na Nafasi ya Sekta ya Madini Katika Mkoa.
Kama ilivyoelekezwa katika ibara ya 64 ya ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020 - 2025 kuwa serikali ya Mkoa itaendelea kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji wanaohitaji kuwekeza katika madini.
Mkoa umebarikiwa kuwa na rasilimali ya madini mbalimbali. Hata hivyo kwa sasa kuna leseni mbili tu za uchimbaji wa kati (Mining Licence) hivyo kupelekea uchimbaji wa madini haya kuwa ni kwa kiasi kidogo na kufanywa na wachimbaji wadogo (Small Scale Miners). Mkoa unatambua umuhimu na nafasi ya madini katika kuchangia pato la taifa na la mwananchi mmoja mmoja. Kwa kulifahamu hilo, mkoa unaweka mazingia mazuri ya upatikanaji wa umeme, uboreshaji wa miundombinu ya barabara na mawasiliano ili kuvutia wawekezaji kuja kuwekeza katika uchimbaji wa madini mbalimbali ndani ya mkoa.
Fursa za uwepo wa madini mbalimbali zimetangazwa kwenye makongamano mbalimbali yaliyofanyika ndani na nje ya Mkoa (Mwaka 2007), Kanda ya Magharibi ya Mikoa ya Rukwa, Katavi na Kigoma (Miaka ya 2012, 2013 na 2014) na Kongamano la Uwekezaji Mkoa wa Rukwa (Mei, 2023). Aidha, maelezo hayo yanapatikana kwenye tovuti ya Mkoa na Halmashauri.
Ofisi ya Madini Mkoa
Katika Mwaka wa Fedha 2018/19, Tume ya Madini ilifungua Ofisi ya Madini Mkoa wa Rukwa (RMO – Rukwa). Ofisi hii imeanza kazi tarehe 09/11/2018 na inasimamia shughuli zote za madini katika Wilaya zote za Mkoa wa Rukwa na Halmashauri zake (Nkasi, Kalambo, Sumbawanga Manispaa na Sumbawanga Vijijini).
Soko la Madini
Ofisi ya Madini Mkoa wa Rukwa kwa kushirikiana Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa tayari imefungua Soko la Madini ambalo lipo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa. Hata hivyo, kuna mpango wa kuhamishia katika jengo la Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga lililopo Mtaa wa Bomani katika Manispaa ya Sumbawanga kwa kuwa kuna nafasi kubwa na karibu zaidi na huduma zingine. Tume ya Madini imeweka vifaa vyote vya kisasa ikiwemo mashine ya XRF na Gemological Tool Kit kwa ajili ya kubaini ubora wa madini mara tu yafikapo sokoni.
Pia Mkoa wa Rukwa una vituo viwili vya ununuzi wa madini (mineral buying centres) katika Bandari ya Kabwe na Kasanga kwa ajili ya kuwahudumia wateja wanaoleta madini kutoka nje ya nchi na pembezoni mwa Ziwa Tanganyika.
Aidha, elimu imeendelea kutolewa kwa wadau wa madini hususan wachimbaji wenye leseni za madini yanayoweza kuuzwa sokoni kuongeza zaidi juhudi za kuzalisha madini ili kuvutia wanunuzi wa kutoka ndani na nje ya nchi. Tume ya Madini Rukwa kwa kushirikiana na Vyombo vya Usalama huwapa vibali wachimbaji wadogo wa madini ya vito kupeleka kwenye masoko mengine hususan Dar es Salaam, Arusha na Dodoma ambako kuna wafanyabiashara wakubwa wa madini hayo hapa nchini.
Makundi ya Madini Yanayopatikana Mkoani Rukwa ni yapi?
Sheria ya Madini Sura 123 imeweka madini katika makundi matano (5). Aidha, Mkoa wa Rukwa umebarikiwa kuwa na makundi yote hayo kama ifuatavyo:
Kundi la Madini ya Vito (gemstones); linajumuisha madini yote ya vito: Ruby, Emerald, Aquamarine, Zircon, nk
Kundi la Madini ya Metali (MM); shaba, titanium, dhahabu, bati, chuma, risasi, manganese, n.k
Kundi la Madini ya Viwandani (IM); Helium, Ulanga, Mawe ya Chokaa, Jasi, Kaoline, nk
Kundi la Madini ya Nishati (energy minerals); Coal
Kundi la Madini ya Ujenzi (BM); Mchanga, Kifusi, Mawe ya Nakshi, nk
Jedwali 1: Mwonekano wa Madini katika Maeneo Mbalimbali Mkoani Rukwa
Na |
Aina ya Madini |
Eneo/Kijiji |
Halmashauri |
1 |
Amethyst
|
Mto Nkomolo, Kasu & Lyazumbi
|
Nkasi
|
2 |
Aquamarine
|
Mlombo
|
Sumbawanga DC
|
3 |
Burma Ruby
|
Katuka
|
Sumbawanga MC
|
Chala & Kantawa
|
Nkasi
|
||
4 |
Dhahabu
|
Mto Mfuizi
|
Kalambo
|
Mto Mkulwe
|
Nkasi
|
||
Mto Kasulisenga
|
Nkasi
|
||
5 |
Diatomite, Helium
|
Bonde la Ziwa Rukwa
|
Sumbawanga DC
|
6 |
Emerald
|
Sumbawanga
|
Sumbawanga MC
|
Mponda
|
Sumbawanga MC
|
||
7 |
Garnets
|
Kantawa, Chala
|
Nkasi
|
8 |
Green Tourmaline
|
Chala, Swaila, Lyele na Tambaruka
|
Nkasi
|
9 |
Kaolin
|
Kufuata Barabara ya Sumbawanga - Kasanga
|
Sumbawanga MC & Kalambo
|
10 |
Kyanite
|
Kizi, Chala na Tambaluka
|
Nkasi
|
11 |
Limonite
|
Mbuga/ Namwele
|
Sumbawanga MC
|
12 |
Maji Moto
|
Chemchem ya Mirumba
|
Kalambo
|
13 |
Maji Moto, Thenardite
|
Chemchem ya Bulongwe
|
Nkasi
|
14 |
Makaa ya Mawe
|
Muze, Namwele
|
Sumbawanga DC
|
Nkomolo
|
Nkasi
|
||
15 |
Mawe (Aggregates)
|
Kamita
|
Sumbawanga MC
|
16 |
Mawe ya chokaa
|
Namwele
|
Sumbawanga DC
|
17 |
Mchanga
|
Mbarika
|
Sumbawanga MC
|
18 |
Moonstone
|
Mkombe Kaskazini mwa Kabwe
|
Nkasi
|
19 |
Piezoelectric Quartz
|
Kijiji cha Matala
|
Nkasi
|
20 |
Rare Earth Elements
|
Mto Kisofi
|
Kalambo
|
21 |
Shaba
|
Mto Hipanga, Mlima Kasola, Mlima Sensika & Ifumwe
|
Nkasi
|
Kasanga na Kapapa
|
Kalambo
|
||
22 |
Shaba, Nikeli
|
Mto Malambo
|
Kalambo
|
23 |
Titanium
|
Kamakanga
|
Kalambo
|
Wipanga
|
Sumbawanga MC
|
||
24 |
Titanium and Zirconium
|
Ntemba na Mkwamba
|
Nkasi
|
25 |
Ulanga
|
Mto Mtose & Mlima Mukwe
|
Kalambo
|
Kipala, Mto Luiche & Chulwe
|
Sumbawanga MC
|
||
Tambaruku
|
Nkasi
|
||
26 |
Zinc
|
Kasanga
|
Kalambo
|
Kirando
|
Nkasi
|
||
27 |
Zircon
|
Nzombo Kijiji cha Matala.
|
Nkasi
|
Mkoani Rukwa Kuna Leseni Ngapi?
Hadi Mwezi Agosti, 2023 Mkoa wa Rukwa ulikuwa na Jumla ya leseni hai zipatazo 249 ambazo zinahusu Utafiti, Uchimbaji wa Kati na Mdogo pamoja na Biashara ya madini kama ilivyoainishwa katika Histogramu.
Kwa mujibu wa takwimu kutoka Ofisi ya Madini Mkoa wa Rukwa uzalishaji wa makaa ya mawe umekuwa ukiongezeka mwaka hadi mwaka ambapo Kampuni ya Edenville International (T) Ltd kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 Jumla ya tani 7,232.99 za makaa ya mawe yenye Thamani ya Shilingi 1,292,195,403.83 zilichimbwa na kuuzwa ndani na nje ya nchi kutoka kwenye mgodi wake wa Kati uliopo Mkomolo Wiayani Nkasi.
Uwepo wa gesi ya Helium katika Mkoa
Taarifa ya tarehe 19 Februari, 2018 kutoka Ofisi ya Madini ya Kanda-Mpanda ilieleza kuwa mwezi Mei, 2016 Kampuni ya Helium One Ltd ilikuwa inamiliki leseni 8 za utafutaji wa Gesi ya Helium Mkoani Rukwa kupitia kampuni zake tanzu za Helium One (Njozi) Limited, Helium One (Gogota) Limited na Helium One (Stahamili) Limited. Katika kazi ilizokuwa imefanya hadi wakati wa kutoa taarifa ilikuwa imegundua uwepo wa Gesi ya Helium Mkoani Rukwa. Kwa mujibu wa makadirio yaliyofanyika, inaonesha kwamba Gesi hii ipo kwa kiasi kisichopungua futi za ujazo Bilioni hamsini na nne (54bcf).
Hadi kufikia Oktoba, 2023 Mkoa wa Rukwa ulikuwa na jumla ya leseni hai 15 za utafiti mkubwa (Prospecting Licences) wa Madini ya Helium ambapo kati ya hizo sita (6) ni za Kampuni ya Rocket Tanzania Limited ambayo imeanza uchorongaji kwenye kisima cha pili (Mbelele 2) baada ya kukamilisha uchorongaji kwenye kisima cha kwanza (Mbelele 1) katika Kijiji cha Zimba. Aidha kampuni ya Helium One (Njozi) Limited nayo inaendelea kufanya kazi ya uchorongaji upande wa Mkoa wa Songwe lengo likiwa ni kuweza kubaini kiasi halisi kilichopo katika maeneo hayo.
Upatikanaji huu wa Gesi ya Helium utachangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya Mkoa wa Rukwa na Nchi kwa ujumla.
Ombi kwa Wawekezaji
Fursa za madini mbalimbali yaliyopo Mkoani Rukwa zinapelekea uhitaji mkubwa wa huduma kwa ajili ya wafanyakazi wa viwanda na machimbo ya madini. Huduma za elimu, vyakula, mawasiliano, hoteli za kisasa, kumbi za mikutano, n.k ni kati ya fursa za kupewa vipaumbele ili wananchi kujiongezea kipato.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa