Ili kufikia Tanzania ya Viwanda elimu ndio uti wa mgongo utakayoifanya Tanzania kufikia azama yake hiyo, hivyo Wizara ya elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia kupitia chuo cha elimu ya Ufundi (VETA) imetenga shilingi Bilioni 7 kwaajili ya ujenzi wa chuo cha ufundi katika Mkoa wa Rukwa.
Akifafanua hayo mtafiti mwandamizi wa masoko ya ajira Julius Paulo Mjelwa amesema kuwa ujenzi wa chuo hicho unategemewa kuanza mwezi wa 9/2017 na kabla ya kukifungua rasmi chuo hicho hupita katika ofisi za Mkuu wa Mkoa kuonana na watendaji wa mkoa ili kujua mahitaji ya mkoa husika katika fani mbalimbali za ufundi.
Hivyo alikutana na watendaji wa ofisi ya mkuu wa mkoa pamoja na halmashauri zake wakiongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa Bernard Makali na kuorodhesha maseomo ambayo wanategemea kuyafundisha mara tu chuo kitakapoanza kufanya shughuli zake.
Masomo waliyopanga kuyafundisha ni pamoja na ufundi wa magari, uchomeleaji vyuma, huduma za vyakula na vinywaji, umeme wa majumbani, usindikaji wa vyakula, ushonaji, ukatibu muktasi, useremala pamoja na ujenzi.
Na chuo hicho kitajengwa katika eneo la msitu wa Muva kwa msaada wa fedha za Benki ya Maendeleo ya Afrika
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa