Kamati ya Siasa Mkoa wa Rukwa ikiongozwa na Hajjat Silafu Jumbe Maufi, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Rukwa imeridhishwa na ubora wa miradi inayotekelezwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga.
Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Rukwa imeanza ziara ya siku nne katika Halmashauri za Mkoa wa Rukwa ikikagua utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka 2020- 2025 katika Mkoa wa Rukwa kuanzia tarehe 24 Julai hadi tarehe 27 Julai 2024.
Wajumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Rukwa wamekagua utekelezaji wa miradi 8 yenye thamani ya shilingi Bilioni 3.1 katika Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga. Miradi iliyokaguliwa ni ujenzi wa Kituo cha Afya Kata ya Senga, ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa Shule ya Msingi Wipanga, ujenzi wa Kituo cha Afya Kata ya Sumbawanga Asilia.
Miradi mingine iliyotembelewa na kukaguliwa ni ujenzi wa Wodi Hospitali ya Manispaa ya Sumbawanga - Isofu, ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Mazoezi Kata ya Chanji, ujenzi wa Shule mpya ya Msingi Sokolo Kata ya Kizwite , ujenzi wa vyumba vya madarasa sita na matundu nane ya vyoo katika Shule ya Sekondari Lwiche na ujenzi wa Vyumba tisa vya Madarasa na matundu vyoo 8 katika Shule ya Sekondari Kizwite.
Kamati imeitaka Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga kuweka katika mipango na bajeti fedha kwa ajili ya kuzijengea uzio Shule zote ili kuimarisha ulinzi kwa wanafunzi na kuzuia uvamizi wa maeneo ya Taasisi za umma.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa