Katika kuhakikisha kuwa mawasiliano ya wananchi wa mikoa miwili katika sekta ya uchumi na uzalishaji yanakuwa serikali ya awamu ya tano imeendelea kuboresha hayo kwa kujenga daraja kubwa lenye urefu wa mita 84 linalounganisha Mkoa wa Rukwa na Songwe kupitia kijiji cha Kilyamatundu, bonde la ziwa rukwa katika mto Momba.
Ujenzi wa daraja hilo ulianza mwanzoni mwa mwezi wa nane mwaka 2017 ambapo ulipaswa kukamilika baada ya miezi 13 yaani mwezi wa nane mwaka huu. Aidha kutokana na changamoto za mafuriko ya mto huo wakati wa mvua za masika, kazi za ujenzi ziliahirishwa na kutegemewa kukamilika mwezi wa pili mwaka 2019.
Ameyasema hayo katibu tawala msaidizi seksheni ya serikali za mitaa Albinus Mgonya wakati wa kuwasilisha taarifa mbalimbali kwa mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ambapo amesema gharama ya ujenzi wa daraja hilo Shilingi Bilioni 17.7.
“Hadi sasa ujenzi umefikia asilimia 65 ambapo tayari mkandarasi amekwishajenga nguzo (pivers) mbili na kingo (abutments) mbili za upande wa Kilyamatundu na Kamsamba pia ujenzi wa beams na sakafu (deck slab) umekamilika,” Alisema
Kukamilika kwa Daraja hili kutaongeza fursa za kiuchumi katika eneo la Bonde la Ziwa Rukwa hivyo kuendelea kuifungua Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga na Mkoa wa Rukwa kwa ujumla.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa