• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Rukwa Region
Rukwa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Rukwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Sumbawanga
    • Wilaya ya Nkasi
    • Wilaya ya Kalambo
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Nkasi
    • H/Wilaya ya Kalambo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Utalii
    • Madini
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Miundombinu ya Rukwa
  • Huduma zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Livestocks
    • Huduma za Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Huduma za Kisheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Fedha
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
    • Waliofaulu na Waliochaguliwa Shule

Daraja la Kisalala

imewekwa Tar: March 17th, 2022



BILIONI 1.8 ZAFANIKISHA UJENZI DARAJA LA KISALALA- RC MKIRIKITI

Na. OMM Rukwa

Katika kuadhimisha mwaka mmoja tangu Serikali ya Awamu ya Sita kuingia madarakani, Wakala wa Barabara mkoa wa Rukwa (TANROADS) umefanikiwa kukamilisha mradi wa ujenzi wa daraja la kimkakati la Kisalala lenye urefu wa mita 35 litakalogharimu shilingi Bilioni 1.89.

Mafanikio hayo yameelezwa jana (16 Machi,2022) na Meneja wa TANROAD Mkoa wa Rukwa Mhandisi Mgeni Mwanga wakati akitoa taarifa kwa Kamati ya Siasa ya CCM mkoa huo ilipokagua utekelezaji wa mradi huo katika kata ya Mnokola iliyopo Mji mdogo wa Laela wilaya ya Sumbawanga.

Mhandisi Mwanga aliongeza kusema Serikali ilitoa fedha mwezi Septemba 2021 ambapo mkandarasi mzawa M/s Mselem Civil Engineering and Contractors Company Ltd wa Sumbawanga alipewa mkataba kwa gharama ya shilingi 1,890,117,000/- na kazi ilichukua miezi sita.

Meneja huyo wa (Wakala wa Barabara) TANROADs mkoa alisema daraja la Kisalala lina urefu wa mita 35 ambapo chanzo cha fedha ni Mfuko wa Barabara na kuwa tayari mkandarasi amelipwa shilingi 1,134,070,200/- huku kazi imefikia asilimia 70 ya utekelezaji.

“Tunamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia shilingi Bilioni 1.89 kwa kazi ya ujenzi wa daraja hili ambalo litakuwa mkombozi kwa wananchi wa kijiji cha Kisalala kuunganishwa na maeneo mengine ambapo mradi huu utakamilika ,Aprili 16, mwaka huu” alisema Mhandisi Mwanga.

Kuhusu manufaa ya mradi huo, Mhandisi Mwanga alisema kukamilika kwa daraja hilo kutakuwa kiungo cha barabara kati ya Mji mdogo wa Laela na vijiji vya Mwimbi, Kizombe na nchi ya jirani ya Zambia.

Akizungumzia mradi huo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Rukwa Rainer Lukala alisema Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya Mkoa imeridhishwa na kasi ya ujenzi wa mradi huo mkubwa na wa kimkakati utakaokuwa mkombozi wa usafiri na uchumi wa wananchi wa Sumbawanga.

Lukala aliwataka wataalam wa TANROAD kuendelea kusimamia kazi za ujenzi wa barabara ili ziwe bora na ziakisi thamani ya fedha iliyotolewa na Serikali ya Chama cha Mapinduzi.

“Kwa daraja hili kwa kulitazama tunaona michango mkubwa wa wakandarasi wazawa kufanikisha miradi na kuwa Serikali ya Chama cha Mapinduzi imetoa fedha nyingi kutatua kero za wananchi. Tanroad tuandalieni ziara ili tukaone mafanikio zaidi kwenye miradi ya miundombinu ili tuweze kuisemea vema kwa wananchi” alisisitiza Lukala.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joseph Mkirikiti alisema kazi ya ujenzi wa miundombinu kufungua maeneo yaliyojifunga inaendelea vema kutekelezwa na TANROAD pamoja na TARURA.

Kuhusu daraja hilo la Kisalala, Mkirikiti alisema ni muhimu kwani liko katika barabara inayoungaisha Sumbawanga na nchi ya Zambia hivyo kukamilika kwake kutakuwa ni fursa nzuri wa wafanyabiashara kukuza shughuli za kiuchumi.

Daraja hilo lina kimo cha meta saba (7) na upana wa meta kumi (10) njia za magari na meta tatu (3) njia ya waenda kwa miguu na ujenzi wake utakamilika Aprili 16 mwaka huu.

Mwisho.


Matangazo

  • RATIBA YA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA 2025 April 15, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 04, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • MATOKEO YA DARASA LA NNE 2024 January 04, 2025
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONGORO AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO, ARIDHISHWA NA KASI YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA UMEME

    May 05, 2025
  • JAMII YAASWA KUJENGA UTAMADUNI WA KUWAHUDUMIA WAZEE

    March 19, 2025
  • KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA TAMISEMI YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI MKOA WA RUKWA

    January 09, 2025
  • RAIS SAMIA ATOA ZAWADI ZA MSIMU WA SIKUKUU WA MWAKA MPYA KWA WATOTO YATIMA NA WENYE MAHITAJI MAALUM MKOANI RUKWA

    December 31, 2024
  • Angalia Zote

Video

LIVE- WAZIRI MCHENGERWA ANATAO TANGAZO LA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Miundombinu ya Rukwa
  • Uvuvi
  • Mikakati ya Mkoa
  • Industries
  • Madini
  • Speeches
  • Huduma za Kilimo
  • Regional History
  • Hotuba

Viunganishi Linganifu

  • Pakua Salaryslip yako hapa
  • Idara ya Takwimu (NBS)
  • Mfumo wa Kutuma, Kupokea na kufuatilia Malalamiko, Mapendekezo, Maulizo na Pongezi
  • Watumishi portal
  • Tafuta ajira Serikalini
  • Pata kila kitu kutoka serikalini

World visitors tracker

world map hits counter

Wapitiaji

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa