• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Rukwa Region
Rukwa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Rukwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Sumbawanga
    • Wilaya ya Nkasi
    • Wilaya ya Kalambo
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Nkasi
    • H/Wilaya ya Kalambo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Utalii
    • Madini
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Miundombinu ya Rukwa
  • Huduma zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Livestocks
    • Huduma za Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Huduma za Kisheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Fedha
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
    • Waliofaulu na Waliochaguliwa Shule

FORODHA

imewekwa Tar: July 28th, 2021

RC MKIRIKITI AAGIZA FORODHA KILANGAWANA SUMBAWANGA KUANZA KAZI

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joseph Joseph Mkirikiti leo (28.07.2021) ametatua mgogoro uliodumu kwa miaka 27 baina  ya wananchi na   pori la akiba Uwanda ambapo wananchi wamekuwa wakizuiwa kupita kwenye pori la akiba la hifadhi wanapokwenda kuvua samaki  Ziwa Rukwa.

Mkirikiti ametoa agizo hilo alipokuwa akiongea na mamia  ya vijana na wananchi wa  kijiji cha Kilangawana na Ilambo kata ya Kilangawana   ambapo ameiagiza halmashauri ya Sumbawanga na hifadhi ya pori la akiba la Uwanda (TAWA) kuanzisha kituo cha forodha kwa ajili ya kukata vibali na ushuru kwenye kijiji hicho hatua itakayoondoa usumbufu wa watu.

"Kuanzia sasa awepo Afisa Uvuvi hapa Kilangawana atoe huduma ya forodha kwa wavuvi bila kikwazo, nataka TAWA msisumbue wananchi wenye vibali" alisema Mkirikiti

Kijiana Frank Solokoto wa kijiji cha Ilambo alisema kero ya ukosefu wa forodha inawafanya wasafiri umbali mrefu kilometa 40 hadi kijiji cha Legeza kufuata huduma ya forodha na  pia imesababisha askari wa pori la akiba Uwanda kuwakamata na kunyang'anya pikipiki na kudaiwa rushwa.

"Mhe. Mkuu wa mkoa mwaka Jana nilikuwa natoka kuvua samaki nikapita njia inayokatiza kwenye hifadhi ya Uwanda nikakamatwa wakaninyang'anya pikipiki, baada ya kuwapa kiasi  wakaniachia ila wakabaki na pikipiki, kwa kuwa kazi yangu ni kuvua samaki nikatafuta pikipiki ingine ambayo nayo walinikamata nayo, pikipiki hizo zimeuzwa na mahakama, sina kazi hapa sina pesa hata mia ya matumizi naomba msaada wako mkuu!!." Alisema Frank.

Mkuu wa mkoa huyo baada ya kusikia kilio hicho alimuita Frank na kumpatia shilingi elfu kumi ya matumizi papo hapo huku wananchi wakishangilia kwenye mkutano wa hadhara.

Frank alimshukuru Mkuu wa mkoa na kukiri makosa ya kupita hifadhini kinyume cha Sheria na kuomba ili kuondoa tatizo la wananchi kukamatwa hifadhini serikali ifungue forodha ya Kilangawana.

"Mkuu wa mkoa ahsante sana, forodha ya Kilangawana ikifunguliwa tutaokoa mapato na kuwasaidia wananchi kuondokana na changamoto ya kukamatwa na wahifadhi wa Uwanda, naomba forodha ifunguliwe ya Kilangawana." Alisema Frank.

Maombi hayo yalipata Baraka ya Kaimu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga Apolinary Macheta ambaye alimueleza mkuu wa mkoa mkutanoni hapo kuwa hata halmashauri iliwahi kupokea malalamiko hayo na kuyawasilisha kwa maandishi katika ofisi ya maliasili lakini hawajajibu.

Mkuu huyo wa Mkoa yupo kwenye ziara ya kazi kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo ikiwemo kutoa elimu ya kujikinga na UVIKO-19 kwenye Halmashauri za mkoa wa Rukwa.

Mwisho

Matangazo

  • RATIBA YA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA 2025 April 15, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 04, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • MATOKEO YA DARASA LA NNE 2024 January 04, 2025
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONGORO AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO, ARIDHISHWA NA KASI YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA UMEME

    May 05, 2025
  • JAMII YAASWA KUJENGA UTAMADUNI WA KUWAHUDUMIA WAZEE

    March 19, 2025
  • KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA TAMISEMI YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI MKOA WA RUKWA

    January 09, 2025
  • RAIS SAMIA ATOA ZAWADI ZA MSIMU WA SIKUKUU WA MWAKA MPYA KWA WATOTO YATIMA NA WENYE MAHITAJI MAALUM MKOANI RUKWA

    December 31, 2024
  • Angalia Zote

Video

LIVE- WAZIRI MCHENGERWA ANATAO TANGAZO LA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Miundombinu ya Rukwa
  • Uvuvi
  • Mikakati ya Mkoa
  • Industries
  • Madini
  • Speeches
  • Huduma za Kilimo
  • Regional History
  • Hotuba

Viunganishi Linganifu

  • Pakua Salaryslip yako hapa
  • Idara ya Takwimu (NBS)
  • Mfumo wa Kutuma, Kupokea na kufuatilia Malalamiko, Mapendekezo, Maulizo na Pongezi
  • Watumishi portal
  • Tafuta ajira Serikalini
  • Pata kila kitu kutoka serikalini

World visitors tracker

world map hits counter

Wapitiaji

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa