• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Rukwa Region
Rukwa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Rukwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Sumbawanga
    • Wilaya ya Nkasi
    • Wilaya ya Kalambo
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Nkasi
    • H/Wilaya ya Kalambo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Utalii
    • Madini
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Miundombinu ya Rukwa
  • Huduma zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Livestocks
    • Huduma za Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Huduma za Kisheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Fedha
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
    • Waliofaulu na Waliochaguliwa Shule

Halmashauri Toeni Fedha za Lishe

imewekwa Tar: March 2nd, 2022

HALMASHAURI TOENI FEDHA KUTEKELEZA AFUA ZA LISHE- RC MKIRIKITI

Na .OMM Rukwa

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joseph Mkirikiti amezionya halmashauri za mkoa huo kwa kutokutoa fedha za utekelezaji wa afua za lishe katika kipindi cha Octoba hadi Desemba 2021.

Ametoa onyo hilo jana (25.02.2022) wakati akiongoza kikao cha tathmini ya mkataba wa shughuli za lishe kipindi cha Julai hadi Desemba 2012 kilichofanyika mjini Sumbawanga ambapo halmashauri zote nne ziliripotiwa kutoa fedha za lishe asilimia 17.5 tu hatua inayokwamisha shughuli za lishe.

“Leo ndio siku ya mwisho nisisikie kuwa Afisa Lishe anasema hajapewa fedha za kutekeleza shughuli wakati mkoa bado una tatizo la udumavu na utapiamlo .Wakurugenzi nendeni mkabadilike .Suala la lishe ni agenda muhimu kwa uhai wa watu wetu” alisisitiza Mkirikiti.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Katibu Tawala Mkoa ambaye pia ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt. Bonoface Kasululu ilionyesha kuwa halmashauri za Sumbawanga Manispaa, Sumbawanga Vijijini, Nkasi na Kalambo zimetoa asilimia 17 na kupelekea mkoa uwe kwenye rangi nyekundu.

Dkt. Kasululu aliongeza kusema matokeo ya ujumla yanaonesha kuwa mkoa wa Rukwa una wastani wa alama asilimia 87 ambapo kiasi hicho kimechangiwa na kutokutolewa kwa fedha za afua za lishe kwa upande wa halmashauri.

“Asilimia ya bajeti ya halmashauri iliyotumika kutekeleza shughuli za lishe kati ya iliyotengwa rangi nyekundu ni asilimia 17.5 kiashiria hiki kinaendelea kufanya vibaya zaidi ikilinganishwa na matokeo ya asilimia 54 kipidi cha mwaka 2020/2021” alieleza Dkt. Kasululu.

Taarifa ya tathmini kwa kiashiria cha asilimia ya fedha zilizotumika kwa shughuli za lishe katika kipindi cha Julai hadi Desemba 2021 kwenye halmashauri na asilimia zake kwenye mabano Manispaa ya Sumbawanga (0.0), Sumbawanga DC (18.9), Nkasi DC (0.0) na Kalambo DC (47.7) hatua inayofanya mkoa kuwa na jumla ya asilimia 17.5

Mmoja wa Maafisa Lishe toka Halmashauri ambaye hatuka jina litajwe alisema “tumekuwa tukiandika madokezo kuomba fedha za shughuli za lishe lakini hatupatiwi bila kupewa sababu. Octoba –Desemba  2021 niliomba shilingi 800,000 lakini hadi leo sijajibiwa na kazi zimesimama” alisema mtaalam huyo.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Shirika la Jukwaa la Lishe Tanzania (PANITA) Aron Isaack alisema licha ya mkoa wa Rukwa kushika nafasi ya 13 kati 26 mwaka 2020/21 bado kuna changamoto kubwa ya shughuli za lishe kutopewa kipaumbele hatua inayosababisha utapiamlo na udumavu kuendelea.

Isaack aliongeza kuwa kunahitajika utashi wa kisiasa ili kutekelezwa kwa mkataba wa lishe miongoni mwa viongozi na watendaji wa serikali wakiwemo Waganga Wakuu wa Wilaya za Rukwa.

“Tunaishukuru serikali kwa kusimamia suala la lishe hasa kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 iliyotamka suala la lishe kupewa kipaumbele “alisema Isaack.

Kwa mujibu wa taarifa ya lishe iliyotolewa na Wizara ya Kilimo Desemba 2020 ilionesha kuwa mikoa inayoongoza kwa uzalishaji mazao ya chakula ndio ina kiwango kikubwa cha udumavu unaotokana na utapiamlo ikiwemo Rukwa (47.9), Njombe (53.6) na Iringa (47.1).

Mwisho.

Matangazo

  • RATIBA YA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA 2025 April 15, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 04, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • MATOKEO YA DARASA LA NNE 2024 January 04, 2025
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONGORO AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO, ARIDHISHWA NA KASI YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA UMEME

    May 05, 2025
  • JAMII YAASWA KUJENGA UTAMADUNI WA KUWAHUDUMIA WAZEE

    March 19, 2025
  • KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA TAMISEMI YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI MKOA WA RUKWA

    January 09, 2025
  • RAIS SAMIA ATOA ZAWADI ZA MSIMU WA SIKUKUU WA MWAKA MPYA KWA WATOTO YATIMA NA WENYE MAHITAJI MAALUM MKOANI RUKWA

    December 31, 2024
  • Angalia Zote

Video

LIVE- WAZIRI MCHENGERWA ANATAO TANGAZO LA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Miundombinu ya Rukwa
  • Uvuvi
  • Mikakati ya Mkoa
  • Industries
  • Madini
  • Speeches
  • Huduma za Kilimo
  • Regional History
  • Hotuba

Viunganishi Linganifu

  • Pakua Salaryslip yako hapa
  • Idara ya Takwimu (NBS)
  • Mfumo wa Kutuma, Kupokea na kufuatilia Malalamiko, Mapendekezo, Maulizo na Pongezi
  • Watumishi portal
  • Tafuta ajira Serikalini
  • Pata kila kitu kutoka serikalini

World visitors tracker

world map hits counter

Wapitiaji

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa