• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Rukwa Region
Rukwa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania PMO - Regional Administration and Local Government Mkoa wa Rukwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Ugavi
      • KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
      • KITENGO CHA MAENDELEO YA JAMII
  • Wilaya
    • Wilaya ya Sumbawanga
    • Wilaya ya Nkasi
    • Wilaya ya Kalambo
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Nkasi
    • H/Wilaya ya Kalambo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Utalii
    • Madini
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Miundombinu ya Rukwa
  • Huduma zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Livestocks
    • Huduma za Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Huduma za Kisheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Fedha
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
    • Waliofaulu na Waliochaguliwa Shule

HALMASHAURI YA WILAYA YA SUMBAWANGA YAIBUKA KINARA WA MKOA UTEKELEZAJI WA AFUA ZA LISHE KWA KIPINDI CHA MWAKA 2022/2023

imewekwa Tar: July 25th, 2023


Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga imeibuka kinara wa utekelezaji wa Afua za Lishe kwa kipindi cha Mwaka 2022/2023 na kukabidhiwa cheti cha pongezi na Mkuu wa Mkoa, Mheshimiwa Charles Makongoro Nyerere. Halmashauri hiyo imeongoza katika kwa kutenga fedha na kusimamia utekelezaji mipango na bajeti ya lishe.  Fedha zilizotumika katika masuala ya lishe katika Halmashauri ya Wilaya hiyo kwa Mwaka 2022/23 ni asilimia 128.

Akikabidhi cheti cha pongezi kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Bi. Lightness Msemo, Mheshimiwa Makongoro ameitaja Halmashauri hiyo kama mfano wa kuigwa katika utekelezaji wa Mkataba wa Lishe  na kueleza kuwa Mkoa wa Rukwa unaweza kuwa wa kwanza katika masuala  mengine pia ikiwa yatapewa kipaumbele kama ilivyofanyika kwa suala la lishe katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga.

Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa amezitaka Halmashauri zote kutenga fedha na kuhakikisha fedha zilizotengwa zinatumika kwa kuzingatia mipango iliyowekwa. Amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri zingine zote za Mkoa wa Rukwa kujifunza na kuiga mbinu zinazotumiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga.

Akihitimisha hafla hiyo Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa amezielekeza Halmashauri zote za Mkoa wa Rukwa kusimamia ipasavyo mipango na bajeti zilizowekwa. Ametaka kusimamiwa kwa mpango wa shule kuwa na mashamba na bustani za mbogamboga ili kusaidia upatikanaji wa chakula bora kwa wanafunzi huku akaielekeza kuongezwa kwa viini lishe katika chakula kinachosambazwa na wazabuni wa shule na huku akisisitiza kutungwa kwa Sheria Ndogo za lishe kwa kila Halmashauri.

Matangazo

  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2026 December 06, 2025
  • RATIBA YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE August 20, 2025
  • RATIBA YA MTIHANI WA UPIMAJI WA KIDATO CHA PILI 2025 November 05, 2025
  • RATIBA YA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI 2025 August 20, 2025
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • WATUMISHI WA AFYA RUKWA WAHIMIZWA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI KUHUSU BIMA YA AFYA KWA WOTE

    December 17, 2025
  • BODI YA USHAURI YA HOSPITALI YA RUFAA SUMBAWANGA YAZINDULIWA, YAAGIZWA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA MENEJIMENTI KUBORESHA HUDUMA.

    November 28, 2025
  • PPRA YAANZA MAFUNZO KUWEZESHA MAKUNDI MAALUM KUSHIRIKI UNUNUZI WA UMMA

    December 25, 2025
  • RC MAKONGORO AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA AMANI RUKWA , ASISITIZA UOMJA NA KULINDA AMANI KWA MAENDELEO YA MKOA

    November 20, 2025
  • Angalia Zote

Video

LIVE- WAZIRI MCHENGERWA ANATAO TANGAZO LA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Miundombinu ya Rukwa
  • Uvuvi
  • Mikakati ya Mkoa
  • Industries
  • Madini
  • Speeches
  • Huduma za Kilimo
  • Regional History
  • Hotuba

Viunganishi Linganifu

  • Pakua Salaryslip yako hapa
  • Idara ya Takwimu (NBS)
  • Mfumo wa Kutuma, Kupokea na kufuatilia Malalamiko, Mapendekezo, Maulizo na Pongezi
  • Watumishi portal
  • Tafuta ajira Serikalini
  • Pata kila kitu kutoka serikalini

World visitors tracker

world map hits counter

Wapitiaji

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa