Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga yapongezwa na Mwenge wa Uhuru 2023 kwa kutumia mapato ya ndani kuteleza Miradi ya Maendeleo.Akiweka jiwe la Msingi kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 Ndg. Abdalla Shaib Kaim katika mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya Kaengesa ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kwa kufanikisha ujenzi wa Kituo hicho kwa mapato ya ndani
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 Ndg Abdalla Shaib Kaim na hadhara ya wananchi wa Wilaya ya Sumbawanga katika viwanja vya Kituo cha Afya Kaengesa ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kwa kutekeleza mradi huo kwa viwango na ubora , ambapo Halmashauri ya Wilaya Ya Sumbawanga imedhamiria kwa dhati kuhakikisha kuwa huduma za afya zinaboreshwa katika Kata ya Kaengesa na wananchi wanapatahuduma za afya zinazotakiwa na kwa ubora unaotakiwa
Aidha amemshukuru Rais Wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha nyingi katika Manispaa ya Sumbawanga ambazo zimewezesha utekelezaji wa miradi mbalimbali katika Halmashauri hiyo na nchi nzima kwa ujumla.
Mwenge wa Uhuru 2023 katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga umezindua Miradi 03,umeweka mawe ya msingi miradi 03 na kukagua miradi miradi 03, Miradi hiyo ni kuweka jiwe la msingi mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Afya Kaengesa wenye thamani ya ya shilingi milioni 270,kuweka jiwe la msingi mradi wa Maji Kalambanzite wenye thamani ya Shilingi bilioni 6, kuweka jiwe la msingi ujenzi wa shule mpya ya Msingi Tuwi yenye thamani ya shilingi milioni 538 Kukagua mradi wa Ujenzi wa Daraja la Mawe Barabara ya Kalambanzite – Kapoka yenye thamani ya shilingi milioni 49
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa amewataka wananchi kutelekeza kauli Mbiu ya Mwenge wa Uhuru 2023 isemayo “Tunza Mazingira, Okoa vyanzo vya Maji kwa Ustawi wa Viumba Haina Uchumi wa Taifa” kwa kitendo, kushiriki katika mapambano ya rushwa, kutokomeza ukatili wa kijinsia na unyanyapa, kuzingatia kanuni za lishe bora ili kuimarisha lishe, kutokomeza maralia na kukakikisha tunaokoa kizazi chetu dhidi ya madawa ya kulevya kwa kukabiliana na changamoto za madawa ya kulevya kwa wakati wote kwa ustawi wa jamii.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa