Sumbawanga
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imewataka Watendaji wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo kutoka mikoa ya Rukwa na Katavi kuzingatia viapo vyao, maadili, weledi na uzalendo katika utekelezaji wa majukumu yao.
Wito huo umetolewa Julai 22, 2025 na Mratibu wa Mafunzo hayo Bi. Tumaini Ng’unga kwa niaba ya Mjumbe wa Tume, Mhe. Magdalena Rwebangira, wakati akifunga mafunzo ya siku tatu yaliyofanyika mjini Sumbawanga.
Bi. Ng’unga ameeleza kuwa ukiukwaji wa viapo ni kosa la kisheria chini ya Sheria ya Uchaguzi Na. 1 ya 2024 na Sheria ya Tume ya Uchaguzi Na. 2 ya 2024, akionya kuwa hatua za kinidhamu zitachukuliwa kwa watakaokiuka.
Aidha, amewataka Watendaji kuwa makini wanapotoa taarifa kwa vyombo vya habari ili kuepusha upotoshaji au taharuki kwa wananchi, akisisitiza umuhimu wa kushirikiana na kuhakikisha taarifa ni sahihi kabla ya kuzisambaza.
Mafunzo hayo ni sehemu ya maandalizi ya Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu, yakilenga kuwajengea uwezo watendaji kuhusu sheria, taratibu na miongozo ya uchaguzi.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa