• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Rukwa Region
Rukwa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania PMO - Regional Administration and Local Government Mkoa wa Rukwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Ugavi
      • KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
      • KITENGO CHA MAENDELEO YA JAMII
  • Wilaya
    • Wilaya ya Sumbawanga
    • Wilaya ya Nkasi
    • Wilaya ya Kalambo
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Nkasi
    • H/Wilaya ya Kalambo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Utalii
    • Madini
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Miundombinu ya Rukwa
  • Huduma zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Livestocks
    • Huduma za Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Huduma za Kisheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Fedha
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
    • Waliofaulu na Waliochaguliwa Shule

Jaji Mkuu awaagiza viongozi wa Mahakama kusimamia usajili wa kesi mitandaoni

imewekwa Tar: November 14th, 2019

Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amewataka Majaji, Naibu Wasajili, Watendaji na Mahakimu wote nchini kutumia mamlaka yao ya usimamizi kuhakikisha wanakagua mfumo wa kusajili na kuratibu mashauri (JSDS II) ili kuona namna mashauri yanavyosajiliwa na kurekebisha endapo kuna makosa.

Jaji Mkuu ametoa agizo hilo kufuatia hatua ya Mahakama ya Tanzania ya kuamua kufanya shughuli zake kwa kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) na kutaka kuacha kupokea takwimu zake kwa njia ya makaratasi na badala yake,  itakuwa ikizisoma takwimu hizo kwa njia ya mtandao.

“Mwaka huu utakuwa ni mwaka wa mwisho kwa Mahakama kupokea takwimu kwenye makaratasi, tutakuwa tukizisoma moja kwa moja kwenye mtandao”, alisema Jaji Mkuu alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari wakati akifanya majumuisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tatu katika mikoa ya Songwe na Rukwa.

“Lengo ni kwenda katika Mahakama ya karne ya 21, Mahakama inayotegemea zaidi mtandao kuliko kutegemea makaratasi”, alisema.

Alisema mfumo wa kusajili na kuratibu mashauri utawawezesha viongozi wa Mahakama kujua ni mashauri mangapi yamesajiliwa nchini, mangapi hayajapangiwa Majaji na Mahakimu, na mangapi yamezidi muda wa kuwepo Mahakamani na hivyo kufuatilia kwa urahisi.

Kwa mujibu wa Jaji Mkuu, mfumo wa JSDS II utasaidia kuzidisha uwazi katika shughuli za Mahakama na kuongeza imani zaidi ya wananchi kwa Mhimili huo.

Alisema Mahakama imedhamiria kuingia katika Tehama ambapo mwezi Julai mwaka huu iliingia Mkataba wenye thamani ya Sh. bilioni 4.1 na Shirika la Mawasiliano ya Simu Tanzania (TTCL) utakaowezesha Mahakama kuingizwa kwenye Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ambapo majengo 157 ya Mahakama nchini yataunganishwa.

Mkataba huo utawezesha kuunganishwa kwa majengo ya Mahakama kuanzia Mahakama ya Rufani, Mahakama Kuu, Mahakama za Hakimu Mkazi, Mahakama za Wilaya na baadhi ya Mahakama za Mwanzo zenye majengo ya kisasa. Mahakama zitakazounganishwa kwenye mtandao huo ni Mahakama ya Rufani 1, Mahakama Kuu 16, Mahakama Kuu Maalumu (Specialized Division 4, Mahakama za Mkoa 29, Mahakama za Wilaya 112 na Mahakama za Mwanzo 10.

Alizitaja faida za Mahakama kusajili mashauri kwa njia ya mtandao kuwa ni pamoja na kuwasaidia mwananchi mwenye shauri Mahakama kufahamu mwenendo mzima wa shauri kwa kujua kila hatua ya shauri lake kwa kufahamu hatua zinazofuata kwenye shauri lake kupitia mtandao.

Jaji Mkuu amehitimisha ziara yake ya kikazi katika mikoa ya Songwe na Rukwa ambapo alikagua shughuli mbalimbali za Mahakama ikiwemo miradi ya ujenzi wa majengo ya mahakama na hali ya utoaji haki kwa ujumla. Katika ziara hiyo, Jaji Mkuu alikagua ujenzi wa majengo ya Mahakama za Mwanzo za Mlowo mkoani Songwe na Mahakama za Mwanzo za Msanzi na Laela mkoani Rukwa.

Lydia Churi-Mahakama, Sumbawanga 

Matangazo

  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2026 December 06, 2025
  • RATIBA YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE August 20, 2025
  • RATIBA YA MTIHANI WA UPIMAJI WA KIDATO CHA PILI 2025 November 05, 2025
  • RATIBA YA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI 2025 August 20, 2025
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • WATUMISHI WA AFYA RUKWA WAHIMIZWA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI KUHUSU BIMA YA AFYA KWA WOTE

    December 17, 2025
  • BODI YA USHAURI YA HOSPITALI YA RUFAA SUMBAWANGA YAZINDULIWA, YAAGIZWA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA MENEJIMENTI KUBORESHA HUDUMA.

    November 28, 2025
  • PPRA YAANZA MAFUNZO KUWEZESHA MAKUNDI MAALUM KUSHIRIKI UNUNUZI WA UMMA

    December 25, 2025
  • RC MAKONGORO AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA AMANI RUKWA , ASISITIZA UOMJA NA KULINDA AMANI KWA MAENDELEO YA MKOA

    November 20, 2025
  • Angalia Zote

Video

LIVE- WAZIRI MCHENGERWA ANATAO TANGAZO LA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Miundombinu ya Rukwa
  • Uvuvi
  • Mikakati ya Mkoa
  • Industries
  • Madini
  • Speeches
  • Huduma za Kilimo
  • Regional History
  • Hotuba

Viunganishi Linganifu

  • Pakua Salaryslip yako hapa
  • Idara ya Takwimu (NBS)
  • Mfumo wa Kutuma, Kupokea na kufuatilia Malalamiko, Mapendekezo, Maulizo na Pongezi
  • Watumishi portal
  • Tafuta ajira Serikalini
  • Pata kila kitu kutoka serikalini

World visitors tracker

world map hits counter

Wapitiaji

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa