• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Rukwa Region
Rukwa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Rukwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Sumbawanga
    • Wilaya ya Nkasi
    • Wilaya ya Kalambo
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Nkasi
    • H/Wilaya ya Kalambo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Utalii
    • Madini
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Miundombinu ya Rukwa
  • Huduma zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Livestocks
    • Huduma za Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Huduma za Kisheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Fedha
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
    • Waliofaulu na Waliochaguliwa Shule

JAMII ISHIRIKIANE NA WALIMU KUKUZA TAALUMA

imewekwa Tar: February 16th, 2023

JAMII ISHIRIKIANE  NA WALIMU KUINUA TAALUMA

Na OMM Rukwa

 Jamii imetakiwa kutoa ushirikiano kwa walimu ili kuleta ufanisi utakaochangia  kuboresha taaluma ya wanafunzi  wa madarasa ya awali na la kwanza kwenye shule za msingi za umma .

Kauli  mbalimbali zimetolewa Februari 14,2023  na walimu wanaoshiriki mafunzo ya kuwajengea uwezo na mbinu za ujifunzaji na ufundishaji KKK yanayotolewa  na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia  kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania wilayani Nkasi.

Shule Bora ni programu ya serikali inayolenga  kuinua ubora wa elimu jumuishi,mazingira salama ya kujifunzia kwa wasichana na wavulana kwenye shule za umma nchini Tanzania na inafadhiliwa na Shirika la Misaada la Uingereza (UKaid) kutoka Serikali ya Uingereza.

Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Kirando iliyopo Nkasi Gerald Kossamu amesema wazazi na serikali wanatakiwa kuungana kuondoa tatizo la uhaba wa vyumba vya madarasa na upungufu wa walimu unaoathiri ufundishaji.

Kossamu alisema shule yake ina changamoto ya wingi wa wanafunzi ambapo hadi kufikia (jana ) Februari  13 mwaka  huu shule imeandikisha jumla ya wanafunzi wa elimu ya awali 443 na wanafunzi 601 wa darasa la kwanza.

“Msongamano ni mkubwa madarasani ambapo shule ina wanafunzi 3,174 na walimu 23 ambao hawatoshi . Walimu inawawia ugumu katika ufundishaji hata namna ya kudhibiti utoro.Serikali itusaidie madarasa ya kutosha” alisema Mwalimu Kossamu.

Happiness Aristides ni mwalimu wa taaluma toka shule ya msingi Mteta iliyopo Laela, halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga alisema wazazi na walezi washirikishwe ili waweze kudhibiti utoro wa watoto unaochangia kufeli .

Kwa upande wake Mratibu wa Programu ya Shule Bora Tanzania  toka Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) Mwesiga  Kabigumila alisema lengo la mafunzo kwa viongozi hao wa walimu ni kuwajengea mbinu na uwezo wa kumudu na kutambua  tabia za wanafunzi na jinsi ya kuwahudumia.

“Ni bora walimu wakuu, wasimamizi wa shule na maafisa elimu   kujikita katika utoaji taarifa sahihi ili kusaidia taifa na mradi wa Shule Bora kuweka mikakati ya   suala  la ujifunzaji na ufundishaji KKK” alisisitiza Mwesiga.

Programu ya Shule Bora imeendesha mafunzo ya uboreshaji wa ufundishaji na ujifunzaji wa darasa la awali, la kwanza na la pili ambapo leo ilikuwa zamu ya kundi la pili  walimu wakuu, walimu wa taaluma, waratibu elimu kata na waelimisha rika toka shule arobaini (40) za msingi za mkoa wa Rukwa.

Mwisho.

Matangazo

  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2025 July 08, 2025
  • RATIBA YA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA 2025 April 15, 2025
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA - 2025, KULINGANA NA MATOKEO YALIYOTANGAZWA NA BARAZA LA MITIHANI LA TAIFA (NECTA) June 04, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 04, 2025
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONGORO ATEMBELEA FORODHA YA KASESYA, AHAMASISHA UWEKEZAJI

    July 15, 2025
  • RC MAKONGORO AFUNGUA JENGO JIPYA LA TAWI LA TCB SUMBAWANGA, APONGEZA KUIMARIKA KWA HUDUMA ZA KIFEDHA.

    July 10, 2025
  • UFAULU KIDATO CHA SITA; RUKWA YAZIDI KUPAA, RC MAKONGORO APONGEZA

    July 10, 2025
  • SERIKALI YAPIGA MARUFUKU TOZO ZA CHANJO NA UTAMBUZI WA MIFUGO

    July 10, 2025
  • Angalia Zote

Video

LIVE- WAZIRI MCHENGERWA ANATAO TANGAZO LA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Miundombinu ya Rukwa
  • Uvuvi
  • Mikakati ya Mkoa
  • Industries
  • Madini
  • Speeches
  • Huduma za Kilimo
  • Regional History
  • Hotuba

Viunganishi Linganifu

  • Pakua Salaryslip yako hapa
  • Idara ya Takwimu (NBS)
  • Mfumo wa Kutuma, Kupokea na kufuatilia Malalamiko, Mapendekezo, Maulizo na Pongezi
  • Watumishi portal
  • Tafuta ajira Serikalini
  • Pata kila kitu kutoka serikalini

World visitors tracker

world map hits counter

Wapitiaji

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa