Mwenyekiti wa Kamati ya Amani Mkoani Rukwa Askofu Ambele Mwaipopo wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Ziwa Tanganyika Mikoa ya Rukwa na Katavi amemuomba Mkuu wa Mkoa huo Mh. Joachim Wangabo kufikisha salamu za pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kupita kwa kishindo katika Uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 pamoja na kuiongoza vuzuri nchi ya Tanzania.
Akizungumza hayo kwa niaba ya Kamati hiyo iliyofanya uchaguzi wake na kupata viongozi wapya Askofu Mwaipopo alisema kuwa viongozi wa dini wanaimani naye kwa yale aliyoyaonesha katika kipindi cha awamu hya kwanza ya uongozi wake na kuendeleza katika kipindi cha awamu yake ya pili.
“Sisi viongozi wa dini tuna Imani nay eye kabisa kwa yale ambayo ameyaonesha kwa kipindi kile cha kwanza na jinsi wanavyokwenda katika uongozi huu naona wameanza vizuri n ani mengi wala hatusemi semi maneno tu, kama viongozi wa dini tunaona Tanzania yetu ikikimbia hasa hta kufikia uchumi wa kati jambo ambalo limemfurahisha kila mmoja wetu,” Alisema.
Aidha wakati akitoa nasaha zake kwa viongozi hao wa dini kabla ya uchaguzi wa uongozi mpya wa Kamati ya Amani mkoani humo Mkuu huyo wa mkoa amewaomba viongozi hao wa dini kuendeleza mshikamano baina yao ili kuirahisishia serikali kuweza kushirikiana nao katika masuala ya msingi ya kiutawala na hatimae nchi iendelee kubaki na amani.
Mh. Wangabo alisema kuwa Pamoja na kuwa dini hizo zina itikadi tofauti za kiimani lakini wote wanamuabudu Mwenyezi Mungu na hivyo inawapasa kuwa Pamoja kwa mambo yale ambayo yanaonekana ni ya kushirikishana.
“Kwahiyo ni alzima na ninyi muwe kitu kimoja, muwe Pamoja, kwahiyo ninaposema serikali ishirikiane na viongozi wa dini kwa upande mmoja na upande wa pili viongozi wa dini wenyewe kwa wenyewe muwe na ushirikiano wa kustosha, hapo tutafika, kama hakuna ushirikiano wa ninyi viongozi wa dini, sasa mtashirikianaje na serikali? Huo ushirikiano utakuwa ni mgumu utakuwa ni kitendawili,” Alihoji.
Katika hiyo ya Amani inaongozwa na aliyechaguliwa kuwa Mwenyekiti Askofu Ambele Mwaipopo wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Ziwa Tanganyika Mikoa ya Rukwa na Katavi, Makamu Mwenyekiti ni Shekh Rashid Akilimali, Shekh wa Mkoa wa Rukwa kutoka Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Katibu ni Mchungaji Emanuel Sikazwe wa Kanisa la Monravian Sumbawanga Pamoja na Katibu Msaidizi Ustadh Mohamed Adam kutoka BAKWATA.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa