• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Rukwa Region
Rukwa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Rukwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Sumbawanga
    • Wilaya ya Nkasi
    • Wilaya ya Kalambo
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Nkasi
    • H/Wilaya ya Kalambo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Utalii
    • Madini
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Miundombinu ya Rukwa
  • Huduma zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Livestocks
    • Huduma za Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Huduma za Kisheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Fedha
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
    • Waliofaulu na Waliochaguliwa Shule

Kaya 199,766 kupatiwa vyandarua 719,254 kukabiliana na Malaria Rukwa.

imewekwa Tar: May 6th, 2020

Katika hatua kukabiliana na mbu waenezao ugonjwa wa Malaria nchini, Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii jinsia, Wazee na Watoto kwa ushirikiano na Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imeendelea kutekeleza kampeni mbalimbali za kudhibiti Malaria ikiwa ni miongoni mwa hatua za kutokomeza ugonjwa huo hadi kufikia mwaka 2030.

Mwakilishi kutoka Wizara ya Afya Peter Gitanya amesema kuwa Kampeni hiyo ambayo imelenga kugawa vyandaru 719,254 kwa mkoa wa Rukwa ni muendelezo wa kampeni kubwa tatu zilizowahi kufanyika miaka ya 2009, 2010 na 2015/2016 na kuongeza kuwa Bohari ya Dawa (MSD) itahusika na usafirishaji wa vyandarua kutoka maghala yao katika kila mkoa hadi kituo cha ugawaji katika Kijiji ama mtaa husika.

“Halmashauri ambako kampeni itafanyika ni zile halmashauri ambazo zina kiwango cha chini cha umiliki wa vyandarua, chini ya 40%, na pia maambukizi ya malaria yapo katika kiwango cha juu na cha kati, Halmashauri zenye kiwango cha chini cha uwepo wa malaria zilizozungukwa na halmashauri zenye kiwango cha juu na cha kati cha uwepo wa malaria na halmashauri ambazo mpango wa ugawaji wa vyandarua kupitia wanafunzi shuleni haufanyiki,” Alisisitiza.

Katika kusisitiza hilo Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amewataka wahusika wote wa kampeni hiyo kushirikiana kwa karibu katika kufikisha elimu iliyosahihi kwa wananchi juu ya matumizi sahihi ya vyandarua na kuongeza kuwa ili kufanikisha mpango wa serikali kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha tunapambana na maradhi hayo ili kuwa na jamii yenye afya na yenye uwezo wa kuzalisha.

“Mimi nitoe wito tu kwamba ili mpango huu uweze kufanikiwa, tunahitaji tushikamane, tushirikiane kwa nguvu zote, kufikisha elimu iliyosahihi kwa wananchi, vinginevyo tusipotoa elimu kwa nguvu zote na watu wakaelewa tunaweza tukatwanga maji kwenye kinu, kwahiyo jambo kubwa liwe ni elimu, elimu iwafikie wananchi kwa nguvu zote, kama tulivyoanza hapa kushirikishana hivi, tuendelee kushusha kuwashirikisha wadau mbalimbali,” Alisema.

Aidha, aliishauri wizara ya afya na taasisi zilizopo chini ya wizara hiyo kuona namna ya kufanya utafiti juu ya miti shamba inayotumika kufukuza mbu katika baadhi ya maeneo vijijini ili wananchi waweze pia kutumia miti hiyo kwa kuipanda maeneo ya nyumba zao na hatimae kuwafukuza mbu hao.

Kampeni hiyo itagawa vyandarua 7,097,565 katika Halmashauri 50 kutoka katika mikoa 10 nchini ikiwa na lengo la kugawa vyandarua hivyo vyenye dawa kwa walengwa kwa asilimia 100 na Kwa mkoa wa Rukwa kampeni hiyo itagawa vyandaru katika halmashauri zote nne za mkoa kwa kuwatambua walengwa na kuwahamasisha juu ya matumizi na utunzaji wa vyandarua hivyo.

Matangazo

  • RATIBA YA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA 2025 April 15, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 04, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • MATOKEO YA DARASA LA NNE 2024 January 04, 2025
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONGORO AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO, ARIDHISHWA NA KASI YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA UMEME

    May 05, 2025
  • JAMII YAASWA KUJENGA UTAMADUNI WA KUWAHUDUMIA WAZEE

    March 19, 2025
  • KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA TAMISEMI YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI MKOA WA RUKWA

    January 09, 2025
  • RAIS SAMIA ATOA ZAWADI ZA MSIMU WA SIKUKUU WA MWAKA MPYA KWA WATOTO YATIMA NA WENYE MAHITAJI MAALUM MKOANI RUKWA

    December 31, 2024
  • Angalia Zote

Video

LIVE- WAZIRI MCHENGERWA ANATAO TANGAZO LA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Miundombinu ya Rukwa
  • Uvuvi
  • Mikakati ya Mkoa
  • Industries
  • Madini
  • Speeches
  • Huduma za Kilimo
  • Regional History
  • Hotuba

Viunganishi Linganifu

  • Pakua Salaryslip yako hapa
  • Idara ya Takwimu (NBS)
  • Mfumo wa Kutuma, Kupokea na kufuatilia Malalamiko, Mapendekezo, Maulizo na Pongezi
  • Watumishi portal
  • Tafuta ajira Serikalini
  • Pata kila kitu kutoka serikalini

World visitors tracker

world map hits counter

Wapitiaji

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa