Mkoa wa Rukwa tarehe 20 Novemba 2022 ulifanya kongamano maalum la kumwombea na kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayoifanya kusukuma mbele maendeleo ya wananchi.
Kongamano hilo lilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Nazareth uliopo mjini Sumbawanga ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Queen Sendiga aliyeambatana na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwananvua Mlindoko pamoja na Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Rashid Mchatta.
Aidha walikuwepo pia viongozi wa dini , vyama vya siasa na wawakilishi wa wananchi toka wilaya zote tatu za Kalambo, Nkasi na Sumbawanga.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa