Naibu Waziri wa OR TAMISEMI Mh. Josephat Sinkamba Kangege ametoa maagizo 14 kwa Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wote Tanzania bara ili kuboresha upatikanaji bora wa huduma za kijamii katika maeneo yao na kuondoa changamoto zilizopo.
Ametoa maagizo hayo katika majumuisho ya ziara yake ya siku 10 katika mkoa wa Rukwa yaliyowakutanisha watumishi wa Halmashauri Nne za Mkoa wa Rukwa yaliyofanyika katika Ukumbi wa Manispaa ya Sumbawanga ambapo ni makao makuu ya Mkoa huo.
Maagizo hayo yamekuja baada ya Kutembelea miradi kadhaa katika Wilaya tatu za Mkoa na kubaini mambo ambayo yanakwamisha maendeleo ya wananchi wa mkoa huo na taifa kwa jumla.
Yafuatayo maagizo yake.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa