• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Rukwa Region
Rukwa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Rukwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Sumbawanga
    • Wilaya ya Nkasi
    • Wilaya ya Kalambo
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Nkasi
    • H/Wilaya ya Kalambo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Utalii
    • Madini
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Miundombinu ya Rukwa
  • Huduma zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Livestocks
    • Huduma za Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Huduma za Kisheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Fedha
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
    • Waliofaulu na Waliochaguliwa Shule

Madarasa 332 Kujengwa Rukwa

imewekwa Tar: November 30th, 2021



MADARASA 332 KUKAMILIKA IFIKAPO DESEMBA –RC MKIRIKITI

Halmashauri za mkoa wa Rukwa zimetakiwa kuhakikisha miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa kwenye shule za sekondari na msingi chini ya Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO-19 yanakamilika ifikapo Desemba mwaka huu.

“Maelekezo yangu ni kuwa tupo nyuma ya ratiba ya utekelezaji miradi hii hivyo nataka Wakurugenzi wa Halmashauri zote kuongeza kasi ya usimamizi na ufuatiliaji ili fedha zilizotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan zipate matokeo tarajiwa kabla ya Desemba 15 madarasa yote yawe yamekamilika kujengwa” alisema Mkirikiti.

Akiwa kwenye ziara ya kukagua miradi ya elimu na afya kwenye Halmasahauri ya Manispaa ya Sumbawanga (22 Novemba,2021) Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joseph Mkirikiti aliagiza Wakurugenzi kuhakikisha miradi hiyo inakamilika pasipo visingizio kwa kuwa fedha tayari zipo kwenye akaunti zao tangu mwezi Octoba mwaka huu.

Mkirikiti aliongeza kusema, katika kutekeleza miradi hiyo ya ujenzi ni budi halmashauri zikazingatia matumizi sahihi ya fedha kwa kuwa na miradi bora na endelevu ambapo msisitizo vifaa kama saruji, mbao na mabati vinunuliwe kwa kuzingatia bei ya soko.

Aliongeza kusisitiza ushirikishwaji wa kamati za ujenzi kwa kila mradi kulingana na Mwongozo ulitolewa na Ofisi ya Rais Tamisemi ambapo wananchi wanatakiwa kutambua na kushiriki kwenye miradi hii.

Kupitia Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO-19 Mkoa wa Rukwa ulipokea jumla ya shilingi 8,940,000,000 ambapo kati hizo shilingi 6,800,000,000 zitatumika kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 332 ya shule za sekondari na  kwenye vituo shikizi shule za msingi.

“Jumla ya madarasa 259 kwa shule za sekondari yenye thamani ya shilingi 5,180,000,000, vyumba vya madarasa katika vituo shikizi vya shule za msingi 73 yenye thamani ya shilingi 1,460,000,000 na mabweni mawili kwa ajili ya wanafunzi wenye ulemavu yenye thamani ya shilingi 160,000,000 yatajengwa kupitia mradi huu kwenye mkoa wa Rukwa” alisisitiza Mkuu wa Mkoa Mkirikiti.

 Aidha,  kiasi cha shilingi 2,140,000,000 kati Bilioni 8.940  zitatumika kwa ajili ya sekta ya afya kwa ajili ya ujenzi wa majengo (2) majengo ya huduma za dharura (EMD) kwa Milioni 600 na ujenzi jengo moja la huduma za wagonjwa mahututi (ICU) kwa shilingi Milioni 100 wilaya ya Kalambo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mkoa pia utatekeleza ununuzi mashine za Mionzi tatu (3) (X-Ray) kwa shilingi Bilioni 1.26 na ujenzi wa nyumba mbili (2) za watumishi wa afya  Nkasi na Kalambo kwa shilingi Milioni 180.

Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Sekondari Lukangao Robert Kasitu alisema changamoto ya uhaba wa maji inakwamisha kasi ya utekelezaji mradi huku Mkuu wa Shule ya ekondari Itwelele Mwakasege Peter akisema changamoto ni upatikanaji wa vifaa vya viwandani kama saruji na nondo kwa wakati.

Matangazo

  • RATIBA YA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA 2025 April 15, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 04, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • MATOKEO YA DARASA LA NNE 2024 January 04, 2025
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONGORO AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO, ARIDHISHWA NA KASI YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA UMEME

    May 05, 2025
  • JAMII YAASWA KUJENGA UTAMADUNI WA KUWAHUDUMIA WAZEE

    March 19, 2025
  • KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA TAMISEMI YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI MKOA WA RUKWA

    January 09, 2025
  • RAIS SAMIA ATOA ZAWADI ZA MSIMU WA SIKUKUU WA MWAKA MPYA KWA WATOTO YATIMA NA WENYE MAHITAJI MAALUM MKOANI RUKWA

    December 31, 2024
  • Angalia Zote

Video

LIVE- WAZIRI MCHENGERWA ANATAO TANGAZO LA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Miundombinu ya Rukwa
  • Uvuvi
  • Mikakati ya Mkoa
  • Industries
  • Madini
  • Speeches
  • Huduma za Kilimo
  • Regional History
  • Hotuba

Viunganishi Linganifu

  • Pakua Salaryslip yako hapa
  • Idara ya Takwimu (NBS)
  • Mfumo wa Kutuma, Kupokea na kufuatilia Malalamiko, Mapendekezo, Maulizo na Pongezi
  • Watumishi portal
  • Tafuta ajira Serikalini
  • Pata kila kitu kutoka serikalini

World visitors tracker

world map hits counter

Wapitiaji

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa