• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Rukwa Region
Rukwa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Rukwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Sumbawanga
    • Wilaya ya Nkasi
    • Wilaya ya Kalambo
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Nkasi
    • H/Wilaya ya Kalambo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Utalii
    • Madini
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Miundombinu ya Rukwa
  • Huduma zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Livestocks
    • Huduma za Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Huduma za Kisheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Fedha
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
    • Waliofaulu na Waliochaguliwa Shule

Mafanikio ya RUWASA Rukwa

imewekwa Tar: April 12th, 2022

RUWASA YATUMIA BILIONI 16 KUKAMILISHA MIRADI 39 YA MAJI RUKWA

Na OMM Rukwa

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joseph Mkirikiti amepongeza Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Rukwa kwa kufanikiwa kutekeleza miradi 39 ya maji yenye gharama ya shilingi Bilioni 16.6 katika mwaka wa fedha 2021/2022 kwenye mkoa wa Rukwa ikiwa ni juhudi za kumtua mama ndoo kichwani.

Mkirikiti amesema hayo leo (11 Aprili 2022) mjini Sumbawanga wakati akiongea kikao cha wadau wa maji ulioratibiwa na RUWASA mkoani huo ukiwa na lengo la kuwafahamisha wadau hatua zilizofikiwa kwenye utekelezaji bajeti na mipango ya kufikisha huduma za maji vijijini.

 Mkuu huyo wa Mkoa alitaja mafanikio mengine ya RUWASA kuwa ni pamoja na huduma za upatikanaji maji kuongezeka kufikia asilimia 64 vijijini na mjini imefikia asilimia 86 kutokana na kukamilika kwa miradi hiyo 39 kati ya miradi 99 yenye thamni ya shilingi Bilioni 25.5 iliyosainiwa mwaka 2021/22 .

“Niwapongeze RUWASA kwa usimamizi mzuri wa miradi hii ya maji, hatua hii inasaidia wananchi kupata maji safi na salama na kuboresha afya hivyo kuwafanya wananchi waendelee kushiriki vema kwenye utekelezaji shughuli za maendeleo” alisema Mkirikiti

Mkirikiti alibainisha kuwa pamoja na jitihada za serikali kutoa fedha kwa miradi ya maji bado kuna changamoto ya uharibifu wa mazingira hususan vyanzo vya maji ikiwemo shughuli za kilimo ndani ya mita Sitini ya maziwa, mito na mabwawa .

“ Kama kuna fedha imeletwa lazima uhakikishe mradi huo unakamilika , hilo ndio lengo la Rais Samia Suluhu Hassan . Katika hili sihitaji kuona hadithi toka kwa watendaji ndani ya Rukwa” alisisitiza Mkirikiti.

Kwa upande wake Meneja wa RUWASA Mkoa wa Rukwa Mhandisi Boaz Pius alisema lengo la kikao hicho ni kuwaeleza wadau kuhusu juhudi zinazofanya na Wizara ya Maji katika kuondoa kero ya ukosefu wa maji  vijijini.

Mhandisi Boaz aliongeza kusema RUWASA inaandaa mikakati kwa kuunganisha vyombo vya watumie maji kote vijijini ili kuwa na vyombo vichache venye wataalam waliobobea ili wasimamie utoaji huduma badala ya kuwa na idadi kubwa ya vyombo hatua inayoongeza gharama za uendeshaji.

Akitoa mada kuhusu michango wa Vyombo vya Watumia Maji ngazi ya Jamii (CBWSOS) Afisa Maendeleo ya Jamii RUWASA Nanyari Lona alisema kiasi cha shilingi 168,423,720 zimekusanywa na vyombo ambapo kati ya hizo shilingi 127,033,162 zilirudishwa kwenda kuendesha vyombo na matengenezo ya miundombinu ya maji.

Lona alieleza pia mafanikio mengine ni kuwepo kwa mwamko wa jamii kuingiza maji majumbani ambapo asimilia 45 ya kaya vijiji zimeunganisha huduma hiyo pia ajira 101 zimepatikana kati hizo mafundi wapo 60 na wahasibu 41.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Mwenyekiti wa CCM Mkoa   Enos Budodi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa aliwapongeza RUWASA kwa mafanikio waliyoyapata ambayo ni ishara nzuri kuwa Ilani ya Uchaguzi ya CCM inatekelezwa.

Kikao hicho cha wadau wa maji kimehudhuriwa na Wakuu wa Wilaya, Wajumbe wa Kamati ya Usalama Mkoa, wahandisi wa RUWASA, SUWASA, Viongozi wa CCM toka wilaya zote, wakurugenzi na wenyeviti wa halmashauri za Sumbawanga, Nkasi na Kalambo .

Mwisho.

Matangazo

  • RATIBA YA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA 2025 April 15, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 04, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • MATOKEO YA DARASA LA NNE 2024 January 04, 2025
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONGORO AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO, ARIDHISHWA NA KASI YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA UMEME

    May 05, 2025
  • JAMII YAASWA KUJENGA UTAMADUNI WA KUWAHUDUMIA WAZEE

    March 19, 2025
  • KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA TAMISEMI YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI MKOA WA RUKWA

    January 09, 2025
  • RAIS SAMIA ATOA ZAWADI ZA MSIMU WA SIKUKUU WA MWAKA MPYA KWA WATOTO YATIMA NA WENYE MAHITAJI MAALUM MKOANI RUKWA

    December 31, 2024
  • Angalia Zote

Video

LIVE- WAZIRI MCHENGERWA ANATAO TANGAZO LA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Miundombinu ya Rukwa
  • Uvuvi
  • Mikakati ya Mkoa
  • Industries
  • Madini
  • Speeches
  • Huduma za Kilimo
  • Regional History
  • Hotuba

Viunganishi Linganifu

  • Pakua Salaryslip yako hapa
  • Idara ya Takwimu (NBS)
  • Mfumo wa Kutuma, Kupokea na kufuatilia Malalamiko, Mapendekezo, Maulizo na Pongezi
  • Watumishi portal
  • Tafuta ajira Serikalini
  • Pata kila kitu kutoka serikalini

World visitors tracker

world map hits counter

Wapitiaji

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa