• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Rukwa Region
Rukwa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Rukwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Sumbawanga
    • Wilaya ya Nkasi
    • Wilaya ya Kalambo
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Nkasi
    • H/Wilaya ya Kalambo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Utalii
    • Madini
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Miundombinu ya Rukwa
  • Huduma zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Livestocks
    • Huduma za Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Huduma za Kisheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Fedha
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
    • Waliofaulu na Waliochaguliwa Shule

Mafanikio ya TANROAD Rukwa

imewekwa Tar: March 24th, 2022

TANROADS RUKWA YAFANIKISHA UJENZI WA MADARAJA 13

 

Na. OMM Rukwa

Serikali ya Awamu ya Sita katika kipindi chake cha mwaka mmoja tangu kuingia madarakani kupitia Wakala wa Barabara (TANROADs) umefanikiwa kutekeleza kazi za matengenezo ya dharura ikiwemo madaraja 13 katika barabara za mkoa wa Rukwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana wakati wa ukaguzi wa barabara  katika kijiji cha Muze kilichopo katika Bonde la Ziwa Rukwa Wilaya Sumbawanga (22 Machi,2022) Kaimu Meneja wa TANROADS Mkoa wa Rukwa Mhandisi Mgeni Mwanga alisema Serikali ilitoa shilingi 13,864,528,000/- katika mwaka wa fedha 2021/22.

Mafanikio hayo yamekuja ikiwa ni jitihada za serikali kufanya matengenezo ya dharura katika barabara za Rukwa ikiwemo ile ya Kasansa –Muze –Kilyamatundu iliyopo ukanda wa Ziwa Rukwa yenye urefu wa kilometa 179 ambayo iko chini ya Wakala wa Barabara (TANROAD) hatua iliyofanya ipitike bila shida kipindi chote cha mwaka.

“Rais Samia Suluhu Hassan amefanikisha upatikanaji wa fedha katika bajeti ya mwaka 2021/22 kwa ajili ya matengenezo ya dharura ya miundombinu ya barabara ambapo tulifanikiwa kujenga madaraja 13 katika barabara za mkoa wa Rukwa” alisema Mhandisi Mgeni.

Mhandisi Mgeni aliongeza kusema miradi hiyo ya ujenzi imefanyika kwa kutumia wakandarasi wazawa hatua inayosaidia kukuza uchumi wa mkoa na Taifa.

Katika hatua nyingine TANROAD imesema serikali iko katika mpango wa ujenzi wa barabara ya Ntendo –Kazungu yenye umbali wa kilometa 25 na barabara ya Kazungu –Muze yenye urefu wa kilometa 12 kwa kiwango cha lami ambapo ujenzi utaanza mwaka wa fedha 2022/23.

Akizungumzia umuhimu wa barabara ya ukanda wa Ziwa Rukwa Diwani wa Kata ya Zimba tarafa ya Mtowisa ,Ephraim Konta alisema kukamilika kwa miundombinu ya ikiwemo daraja la Lwanji kumesaidia kurahisisha shughuli za kiuchumi kwani mazao yanafika sokoni yakiwa katika ubora .

Diwani huyo aliongeza kusema anaomba serikali kutoa elimu kwa wananchi kuhusu kutofanya shughuli za kilimo na Mifugo katika kingo za mito hatua itakayosaidia madaraja kuwa imara na mito kutokana hama.

Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Solola halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga, Godfrey Tanganyika alishukuru serikali kwa kujenga daraja lililokuwa kikwazo cha kuunganisha kijiji hicho na kijiji cha Ilemba kufuatia mvua kusababisha mto kuhama.

“Tunashukuru serikali kwa kujenga daraja hili pia tunamwomba Rais Samia atuwekee lami katika barabara hii ya ukanda wa Ziwa Rukwa kwani ndio barabara kubwa iliyobaki bila lami” alisema Tanganyika.

Nao wanafunzi Felista Zuberi na Elizabeth Nasri wa kidato cha nne shule ya sekondari Mazoka iliyopo kata ya Muze walisema kukamilika kwa ujenzi wa daraja la Muze kumesaidia waweze kuwa na uhakika wa kuhudhuria masomo muda wote ikiwemo kipindi cha masika.

“Tulikuwa tukikosa masomo kipindi mto huu ulipokuwa ukijaa na njia kukatika kwani tunaishi Muze na shule iko upande wa pili kijiji cha Mazoka kata ya Mbwilo” alisema Felista mwenye umri wa miaka 18.

Wakala wa Barabara (TANROAD) Mkoa wa Rukwa unaendelea na kazi ya kusimamia mtandao wa barabara Kuu za lami zenye urefu wa kilometa 415 .86 kati yake za lami kilometa 298.35 na za changarawe kilometa 117 huku ikisimamia barabara za mkoa zenye urefu wa kilometa 834.98 kati ya hizo za lami ni kilometa 76.83 na za changarawe ni kilometa 758.15

Mwisho

Matangazo

  • RATIBA YA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA 2025 April 15, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 04, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • MATOKEO YA DARASA LA NNE 2024 January 04, 2025
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONGORO AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO, ARIDHISHWA NA KASI YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA UMEME

    May 05, 2025
  • JAMII YAASWA KUJENGA UTAMADUNI WA KUWAHUDUMIA WAZEE

    March 19, 2025
  • KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA TAMISEMI YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI MKOA WA RUKWA

    January 09, 2025
  • RAIS SAMIA ATOA ZAWADI ZA MSIMU WA SIKUKUU WA MWAKA MPYA KWA WATOTO YATIMA NA WENYE MAHITAJI MAALUM MKOANI RUKWA

    December 31, 2024
  • Angalia Zote

Video

LIVE- WAZIRI MCHENGERWA ANATAO TANGAZO LA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Miundombinu ya Rukwa
  • Uvuvi
  • Mikakati ya Mkoa
  • Industries
  • Madini
  • Speeches
  • Huduma za Kilimo
  • Regional History
  • Hotuba

Viunganishi Linganifu

  • Pakua Salaryslip yako hapa
  • Idara ya Takwimu (NBS)
  • Mfumo wa Kutuma, Kupokea na kufuatilia Malalamiko, Mapendekezo, Maulizo na Pongezi
  • Watumishi portal
  • Tafuta ajira Serikalini
  • Pata kila kitu kutoka serikalini

World visitors tracker

world map hits counter

Wapitiaji

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa