Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Charles Makongoro Nyerere amewataka wananchi wanaohitaji kununua ardhi katika maeneo ya vijiji kuzingatia Sheria ya Ardhi ya vijiji wakati wa kununua Ardhi.
Mheshimiwa Makongoro ameyasema hayo tarehe 21 Mei, 2024 alipokuwa akisikiliza kero za wananchi wa Mtowisa alipofanya ziara katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kwa lengo la kukagua miradi na kusikiliza kero za wananchi katika eneo hilo.
Mheshimiwa Charles Makongoro Nyerere amewataka wananchi kuhakikisha wanapotaka kununua maeneo yanayomilikiwa na vijiji kufuata taratibu za manunuzi kwa kuhakikisha kuwa maombi yao yanapitishwa na Mkutano Mkuu wa Kijiji kwa eneo lisilozidi ekari 50.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa