Mheshimiwa Charles Makongoro Nyerere Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ameshiriki sherehe za Siku ya Sheria nchini ( Law Day). Sherehe hizo hufanyika tarehe 01 ya mwezi Februari kila Mwaka.
Maadhimisho hayo yamefanyika katika viwanja vya Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga leo Februari Mosi, 2024 na kuhudhuriwa na uongozi wa Mahakama na wadau wengine wa tasnia ya Sheria Mkoani hapa.
Sherehe hizo zilitanguliwa na Wiki ya Sheria nchini iliyoadhimishwa kuanzia Januari 24 hadi 30, 2024 kwa kutoa elimu na msaada wa kisheria kwa wananchi wa Sumbawanga na viunga vyake. Wiki ya Sheria iliadhimishwa katika eneo la wazi karibu na Soko Kuu la Sumbawanga ambapo watu 5400 walihudumiwa.
Wiki ya Sheria Mwaka 2024 imeadhimishwa ikisindikizwa na kauli mbiu isemayo;
"Umuhimu wa Dhana ya Haki kwa Ustawi wa Taifa: Nafasi ya Mahakama na wadau katika kuboresha mfumo jumuishi wa Haki Jinai"
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa