• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Rukwa Region
Rukwa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Rukwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Sumbawanga
    • Wilaya ya Nkasi
    • Wilaya ya Kalambo
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Nkasi
    • H/Wilaya ya Kalambo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Utalii
    • Madini
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Miundombinu ya Rukwa
  • Huduma zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Livestocks
    • Huduma za Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Huduma za Kisheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Fedha
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
    • Waliofaulu na Waliochaguliwa Shule

Makusanyo Kiduchu Halmashauri Za Mkoa Wa Rukwa Yamchefua Naibu Waziri Mabula

imewekwa Tar: January 24th, 2020

Makusanyo ya kodi ya pango la ardhi katika halmashauri za mkoa wa Rukwa yamemvuruga Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula baada ya kuelezwa kuwa hadi kufikia Desemba 2019 jumla ya shilingi milioni 148.2 zilikusanywa na halmashauri zote nne sawa na asilimia 7.9 .


Akiwa  katika ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi katika mkoa wa Rukwa jana ambapo alikutana na watumishi wa sekta ya ardhi, Dkt Mabula alishangazwa na namna maafisa ardhi wa halmashauri hizo wasivyofuatilia makusanyo ya kodi ya pango la ardhi kiasi cha kuzifanya halmashauri hizo kukusanya kiasi kidogo cha fedha.


Alisema, haiwezekani ndani ya miezi sita halmashauri nne za mkoa wa Rukwa zikusanye asilimia 7.9 ya kodi ya pango la ardhi jambo alilolieleza kuwa linatia mashaka kama halmashauri hizo zitaweza kufikisha hata asilimia hamsini ya makusanyo ya kodi ya pango la ardhi kufikia mwisho wa mwaka wa fedha 2019/2020.


Kwa mujibu wa Taarifa ya mkoa wa Rukwa iliyosomwa na Mrasimu Ramani wa mkoa wa Rukwa Kelvin Mahundi, katika kipindi cha mwaka wa fedha 2019/2020 halmashauri za mkoa huo  zilikadiriwa kukusanya jumla ya sh 1,880,000,000.00 ambapo Manispaa ya Sumbawanga ilikusanya kiasi cha sh. 94,253,273.00, Halmashauri ya wilaya ya Nkasi sh. 16,494,189.00, Kalambo sh 1,793,550.00 na Halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga sh 35,680,575.00 na hadi hadi Desemba 2019 jumla ya shilingi 148,221,587.00 zilikusanywa kwa halmashauri zote sawa na asilimia 7.9.


‘’Wakurugenzi wako busy na masuala mengine, mkoa mzima una silimia 7.9 ya makusanyo ya kodi ya pango la ardhi! ni aibu na hamuwezi kufikia asilimia 50 ya makusanyo naagiza wote mkafanye uhakiki wa wadaiwa wa kodi ya ardhi na muwapelekee ilani ili watakaokaidi wafikishwe kwenye Mabaraza ya Ardhi’’ alisema Dkt Mabula.


Aidha, Naibu Waziri Mabula aliagiza kufikia Machi 2020 lazima kuwe na mabadiliko ya utendaji kazi kwenye sekta ya ardhi kwa halmashauri za mkoa wa Rukwa, vinginevyo atafikiria kama wakuu wa idara wanatosha kuendelea na nafasi zao na kusisitiza kama ni Mkuu wa Idara au Afisa Ardhi Mteule ataondolewa.


Dkt Mabula alisema mikoa yote aliyoitembelea kwenye ziara zake za kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi imefikisha asilimia thelathini ya makusanyo ya kodi ya ardhi lakini mkoa wa Rukwa umemsononesha sana na kumuagiza Kamishna wa Ardhi Msaidizi Kanda Thadei Kabonge atoe maelezo kuhusiana na utendaji kazi wa Wakuu wa idara kama wanafaa kushika nafasi zao.


Hata hivyo, Naibu Waziri Mabula alibainisha kuwa kulingana na taarifa zilizokuwa kwenye mfumo wa kielektronik Manispaa ya Sumbawanga ilitakuwa kukusanya Bilioni 6.7, Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga milioni 20, Kalambo milioni 1.6 na Nkasi milioni 16 hiyo inatokana na halmashauri hizo kuwa na malimbikizo ya wadaiwa kodi ya pango la ardhi. 

Matangazo

  • RATIBA YA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA 2025 April 15, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 04, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • MATOKEO YA DARASA LA NNE 2024 January 04, 2025
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONGORO AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO, ARIDHISHWA NA KASI YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA UMEME

    May 05, 2025
  • JAMII YAASWA KUJENGA UTAMADUNI WA KUWAHUDUMIA WAZEE

    March 19, 2025
  • KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA TAMISEMI YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI MKOA WA RUKWA

    January 09, 2025
  • RAIS SAMIA ATOA ZAWADI ZA MSIMU WA SIKUKUU WA MWAKA MPYA KWA WATOTO YATIMA NA WENYE MAHITAJI MAALUM MKOANI RUKWA

    December 31, 2024
  • Angalia Zote

Video

LIVE- WAZIRI MCHENGERWA ANATAO TANGAZO LA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Miundombinu ya Rukwa
  • Uvuvi
  • Mikakati ya Mkoa
  • Industries
  • Madini
  • Speeches
  • Huduma za Kilimo
  • Regional History
  • Hotuba

Viunganishi Linganifu

  • Pakua Salaryslip yako hapa
  • Idara ya Takwimu (NBS)
  • Mfumo wa Kutuma, Kupokea na kufuatilia Malalamiko, Mapendekezo, Maulizo na Pongezi
  • Watumishi portal
  • Tafuta ajira Serikalini
  • Pata kila kitu kutoka serikalini

World visitors tracker

world map hits counter

Wapitiaji

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa