Rais Samia Suluhu Hassan amezindua vihenge na maghala ya kisasa ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), katika eneo la Kanondo mkoani Rukwa.
Akizungumza na wananchi wa eneo hilo mara baada ya uzinduzi huo Rais Samia ameelekeza kuwa mbolea ya ruzuku iendelee kuwepo na kusisitiza mahindi yanunuliwe kutoka kwa wakulima wa vijijini kwa gharama ya shilingi 600 kwa kilo; na mjini shilingi 650 kwa kilo.
Aidha, amewasisitiza wananchi kutosafirisha mahindi nje ya nchi bila vibali vya Wizara ya Kilimo na taratibu nyingine zinazotakiwa kwa kuwa hatua hiyo inaathiri uchumi na soko la kibiashara.
Kuhusu mizani ya kidigiti Rais Samia ameelekeza ziongezwe kwa wingi katika vituo vya NFRA ili kurahisisha huduma kwa wakulima kwa kupata haki stahiki ya uzito wa mazao yao.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa