Waziri wa Maliasili na Utalii mh. Jumanne Magembe ameeleza umuhimu wa kuimarisha utalii katika Mkoa wa Rukwa kwa kuwa na kivutio kikubwa cha maporormoko ya Mto Kalambo ambapo maporomoko hayo ni ya pili kwa urefu barani Afrika.
Amesema kuwa imefika wakati sasa kuondokana na fikra ya utalii katika mikoa ya kaskazini peke yake na kuamua kuelekeza nguvu za uwekezaji katika mikoa ya kusini na nyanda za juu kusini kama Rukwa na Katavi.
Ameeleza kuwa mikoa hii inavivutio vingi sana na tayari kuna wawekezaji kadhaa ambao wameomba kujenga nyumba za kupumzikia katika maeneo kadhaa ya vivutio yaliyoko katika mikoa ya Katavi na Rukwa.
“Ni Imani yetu kuwa hawa ambao watajenga hizi nyumba za kupumzikia watahitaji watalii wa kuja kuzitumia hivyo kwa kuwatumia wao tunaweza kutangaza maeneo yetu haya ya utalii,” Alimalizia.
Aliamua kueleza mikakati hiyo baada ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kamishna Mstaafu Zelote Stephen kuongelea shauku yake ya kutaka nchi na dunia nzima ifahamu maporomoko ya mto Kalambo ambayo yanapatikana mpakani mwa Tanzania na Zambia.
Hayo yalisemwa wakati Mh. Zelote alipokuwa akitoa historia fupi ya mkoa kabla ya Mh. Magembe kuanza ziara yake ya siku tano katika mkoa wa Rukwa.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa