• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Rukwa Region
Rukwa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Rukwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Sumbawanga
    • Wilaya ya Nkasi
    • Wilaya ya Kalambo
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Nkasi
    • H/Wilaya ya Kalambo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Utalii
    • Madini
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Miundombinu ya Rukwa
  • Huduma zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Livestocks
    • Huduma za Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Huduma za Kisheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Fedha
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
    • Waliofaulu na Waliochaguliwa Shule

MHESHIMIWA MAKONGORO ATOA WITO WA USHIRIKIANO KATIKA KUIMARISHA ELIMU YA LISHE

imewekwa Tar: September 18th, 2025

MHESHIMIWA MAKONGORO ATOA WITO WA USHIRIKIANO KATIKA KUIMARISHA ELIMU YA LISHE


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mheshimiwa Charles Makongoro Nyerere, ametoa wito kwa viongozi wa Serikali, taasisi za dini, jamii na vyombo vya habari kushirikiana kikamilifu katika kutoa elimu ya lishe bora kwa wananchi, ili kusaidia kuimarisha afya na maendeleo ya watoto na vijana.


Akizungumza leo Septemba 18, 2025 katika kikao cha tathmini ya utekelezaji wa Mkataba wa Lishe kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa (RDC), Mheshimiwa Makongoro ameeleza kuwa lishe duni bado ni changamoto kubwa inayoathiri ukuaji wa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano, hali inayochangia udumavu na matatizo ya kiafya kwa watoto katika Mkoa wa Rukwa na taifa kwa ujumla.


"Ni wajibu wa kila kiongozi kutumia kila jukwaa analopata kuwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa lishe bora. Nawaomba viongozi wa dini wasaidie kufikisha ujumbe huu katika nyumba za ibada, wataalamu waendelee kutoa miongozo sahihi ya lishe, na vyombo vya habari viendelee kuelimisha jamii kupitia vipindi na makala,"amesema Mheshimiwa Makongoro.


Licha ya Mkoa wa Rukwa kupata wastani wa asilimia 85 katika tathmini ya kitaifa ya utekelezaji wa afua za lishe, Mheshimiwa Makongoro amebainisha kuwa bado kuna changamoto ya kutotengwa kwa rasilimali fedha za kutosha katika Halmashauri za Mkoa wa Rukwa kwa ajili ya kutekeleza afua hizo muhimu kama ilivyokubaliwa kwenye Mkataba wa Lishe.


Aidha,amewataka wajumbe wa kikao hicho kuhakikisha kuwa mipango na bajeti za lishe zinawekewa vipaumbele katika Mwaka wa Fedha unaofuata, huku akisisitiza kuwa taifa lenye viwango vya juu vya udumavu haliwezi kufikia maendeleo endelevu.


“Tusimame pamoja kama Mkoa kuhakikisha kuwa tunawekeza ipasavyo katika lishe, kwa sababu taifa lenye watoto na vijana wenye udumavu ni taifa lenye changamoto katika nguvu kazi, elimu na uchumi. Ushirikiano wetu ndio msingi wa mabadiliko ya kweli,”amesisitiza Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa.


Kikao hicho kimehudhuriwa na wakuu wa idara, wawakilishi wa Halmashauri zote za Mkoa wa Rukwa, wawakilishi wa taasisi zisizo za kiserikali,viongozi wa dini na wadau mbalimbali wa sekta ya lishe.

Matangazo

  • RATIBA YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE August 20, 2025
  • RATIBA YA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI 2025 August 20, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2025 July 08, 2025
  • RATIBA YA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA 2025 April 15, 2025
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • MBIO ZA MWENGE ZAENDELEA KALAMBO RUKWA, MIRADI YA MAENDELEO YAENDELEA KUMULIKWa

    September 30, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WAPOKELEWA MANISPAA YA SUMBAWANGA, MIRADI YA BILIONI 30.3

    September 29, 2025
  • MWENGE WA UHURU WAWEKA JIWE LA MSINGI SHULE YA AMALI WILAYANI NKASI; KIONGOZI ATAKA WANANCHI WATUMIE FURSA YA ELIMU YA UFUNDI

    September 28, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WAPOKELEWA MKOANI RUKWA; KUKIMBIZWA KWA SIKU NNE; KUMULIKA MIRADI YA BILIONI 55.3

    September 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

LIVE- WAZIRI MCHENGERWA ANATAO TANGAZO LA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Miundombinu ya Rukwa
  • Uvuvi
  • Mikakati ya Mkoa
  • Industries
  • Madini
  • Speeches
  • Huduma za Kilimo
  • Regional History
  • Hotuba

Viunganishi Linganifu

  • Pakua Salaryslip yako hapa
  • Idara ya Takwimu (NBS)
  • Mfumo wa Kutuma, Kupokea na kufuatilia Malalamiko, Mapendekezo, Maulizo na Pongezi
  • Watumishi portal
  • Tafuta ajira Serikalini
  • Pata kila kitu kutoka serikalini

World visitors tracker

world map hits counter

Wapitiaji

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa