Mheshimiwa Charles Makongoro Nyerere, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa amewasili katika kituo chake kipya cha kazi leo Jumatatu ya tarehe 12 Juni 2023.
Mheshimiwa Makongoro aliteuliwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa tarehe 23 Mei 2023.
Baada ya kuwasili amepokelewa na watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Rukwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Rukwa.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa