Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Magdalena Rwebangira, leo amefungua rasmi mafunzo ya Watendaji wa Uchaguzi kutoka mikoa ya Rukwa na Katavi katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.
Mafunzo haya ya siku tatu yanawajumuisha Waratibu wa Uchaguzi wa Mkoa, Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi wa Jimbo, Maafisa Uchaguzi na Maafisa Ununuzi.
Mhe. Rwebangira amewasisitiza washiriki kufuatilia kwa umakini ili waweze kutekeleza majukumu ya uchaguzi kwa ufasaha, uadilifu na weledi.
Mafunzo haya ni maandalizi muhimu kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa, kwa kuhakikisha chaguzi huru, haki na zinazoaminika.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa