Shekhe Mkuu na Mufti wa Tanzania Aboubakar Bin Zuber Bin Ali amepongeza ushirikiano uliopo baina ya baraza la waislamu la Mkoa pamoja na serikali ya Mkoa wa Rukwa katika kutatua kurekebisha au kuyaweka sawa masuala mablimbali kwa maslahi ya watanzania.
“siku zote huwa nawaamnbia viongozi wangu hawa wa baraza kwamba wafanye kila wanachokifanya lakini wahakikishe kuwa wanajenga mahusiano mazuri na serikali ya mahala walipo, baada ya kujenga mahusiano na wananchi wa dini zote basin a serikali pia na katika eneeo hili ninapowauliza panaonesha pana mashirikiano mazuri, cha kusema ni kwamba ushirkinao na uhusiano uendelee na udumu vizuri kwasababu ndio utakaoweza kujenga nchi yetu katika masuala yote ya maendeleo,” alisema.
Wakati akisoma taarifa ya Mkoa, mwakilishi wa mkuu wa Mkoa wa Rukwa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Khalfan Haule amepongeza juhudi mbalimbali zinazofanywa na waislamu katika kuiletea nchi maendeleo na kumuomba mufti wa Tanzania kuikumbuka Rukwa katika mipango yao mbalimbali ya uwekezaji katika sekta ya afya, maji, elimu na viwanda.
“Baada ya serikali kutangaza elimu bure kuna mafuriko ya wanafunzi huko mashuleni, hii inaonesha kwamba bado miundombinu ya elimu bado haitoshelezi hivyo tunahitaji kwenye eneo hilo ushirikinao wa kujenga shule za msingi, sekondari na hata vyuo, sisi ni eneo la pembezoni lakini tunapenda kuliita eneo la kipaumbele hivyo kwenye mipango yako basi utuweke kwenye eneo la kipaumbele,” Alisema.
Mufti wa Tanzania atafanya ziara ya siku mbili katika Wilaya ya Sumbawanga pamoja na Nkasi, akizindua na kuweka mawe ya msingi katika misikiti pamoja na kituo cha afya kilichopo kata ya kirando, Wilayani Nkasi.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa