MIRADI YA SHILINGI BILIONI 4.7 KUTEMBELEWA NA MWENGE WA UHURU RUKWA
Na. OMM Rukwa
Mwenge wa Uhuru umeanza mbio zake kwa mkoa wa Rukwa ambapo jumla ya miradi Kumi na Miwili yenye thamani ya shilingi Bilioni 4.7 itawekewa mawe ya msingi, kukaguliwa na kuzinduliwa katika halmashauri nne za Sumbawanga Vijijini, Kalambo, Manispaa ya Sumbawanga na Nkasi.
Akizungumzia hali ya maandalizi, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Queen Sendiga leo (19.09.2022) katika kijiji cha Kilyamatundu wilaya ya Sumbawanga ukitokea mkoa wa Songwe ambapo alisema wananchi wapo tayari kuupokea Mwenge wa Uhuru na kukimbizwa kwenye maeneo yao.
" Tupo tayari kukimbiza Mwenge wa Uhuru na kwamba tumejiandaa kwa kuwa na miradi iliyokidhi viwango na kuwa utakamilisha salama kazi yake " alisema Sendiga.
Kwa upande wake Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Sahili Geraruma amewasihi watendaji na watumishi wa serikali kuzingatia viwango vya ubora wanaposimamia miradi ya maendeleo.
Geraruma akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kipeta alipweka jiwe la msingi la Kituo cha Afya kilichochengwa kwa fedha tozo ya miamala shilingi Milioni 500 alionya dhidi ya vitendo vya kutozingatiwa vigezo na ucheleweshwaji wa matumizi ya fedha.
"Mradi huu ni mzuri lakini kuna mapungufu kidogo. Kutozingatiwa kwa viwango vya ujenzi ikiwemo BOQ pamoja na kutopata kibali cha TAMISEMI kuhusu maboresho ya ramani yanatia shaka uzalendo wa wataalam wetu wa halmashauri "alisema Geraruma.
Aidha akiwa katika mradi wa shule ya sekondari Katuhura kata ya Laela, Kiongozi huyo wa mbio za Mwenge Kitaifa aliweka jiwe la msingi la mradi huo na kutoa rai kwa watendaji wa halmashauri hiyo kuongeza kasi ili ifikapo mwezi Octoba mwaka huu mradi huo ukamilike na kuanźa kutumika.
Serikali ilitoa fedha shilingi Milioni 470 kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo mpya ya sekondari Katuhura ambapo ujenzi umefikia asiĺimia 70.
Mwenge wa Uhuru leo umekamilisha mbio zake Halmashuri ya Wilaya ya Sumbawanga kwa kukagua , kuweka mawe ya msingi kwenye miradi minne na kuzungumza na wananchi .
Kesho Mwenge wa Uhuru utakimbizwa kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo.
Mwisho.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa