Mwenge wa Uhuru 2023 umezindua mradi 01, umekagua miradi 04 na kuweka mawe ya msingi miradi 02 yenye thamani ya shilingi Bilioni 1.9 Katika Manispaa ya Sumbawanga Mkoni Rukwa.
Akiongea Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 Ndg Abdalla Shaib Kaim na hadhara ya wananchi wa Manispaa ya Sumbawanga katika Viwanja vya Shule ya Msingi Ndua ameipongeza Halmashauri ya Manispaa kwa kutekeleza miradi kwa viwango na ubora unaotakiwa na kusisitiza kuwa maelekezo yote yaliyotolewa yanafanyiwa kazi.
Ndg. Abdalla Shaib Kaim amesema Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga imejipanga na kuhakikisha kuwa huduma za Afya zinaboreshwa kwa kukamilisha wodi 03 za wanawake, wanaume na watoto na chumba cha kuhifadhia maiti ili wananchi waweze kupatiwa huduma sawa na malengo ya Serikali ya Awamu ya Sita.
Aidha Amemshukuru Rais Wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha nyingi katika Manispaa ya Sumbawanga ambazo zimewezesha utekelezaji wa baadhi ya miradi ya maendeleo kama ujenzi wa Wodi 03 katika Hospitali ya Manispaa kiasi cha Shilingi Milioni 750, Ujenzi wa Shule Mpya ya Sokolo kiasi cha Shilingi Milioni 547, Ujenzi wa Barabara kwa kiwango cha Lami (Mtaa wa Kodova)Kiasi cha Shilingi Milioni 314 na mingine mingi katika manispaa ya Sumbawanga na Mkoa wa Rukwa kwa ujumla.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa amewataka wananchi kutelekeza kauli Mbiu ya Mwenge wa Uhuru 2023 isemayo “Tunza Mazingira, Okoa vyanzo vya Maji kwa Ustawi wa Viumba Haina Uchumi wa Taifa” kwa kitendo, kushiriki katika mapambano ya rushwa, kutokomeza ukatili wa kijinsia na unyanyapa, kuzingatia kanuni za lishe bora ili kuimarisha lishe, kutokomeza maralia na kukakikisha tunaokoa kizazi chetu dhidi ya madawa ya kulevya kwa kukabiliana na changamoto za madawa ya kulevya kwa wakati wote kwa ustawi wa jamii.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa