• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Rukwa Region
Rukwa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Rukwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Sumbawanga
    • Wilaya ya Nkasi
    • Wilaya ya Kalambo
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Nkasi
    • H/Wilaya ya Kalambo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Utalii
    • Madini
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Miundombinu ya Rukwa
  • Huduma zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Livestocks
    • Huduma za Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Huduma za Kisheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Fedha
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
    • Waliofaulu na Waliochaguliwa Shule

NFRA

imewekwa Tar: September 1st, 2021

NFRA YANUNUA TANI 4,600 ZA MAHINDI YA WAKULIMA RUKWA

Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula nchini (NFRA) imefanikiwa kununua tani 4,600 za mahindi zenye thamani ya Shilingi Bilioni Mbili na Milioni Mia tatu toka kwa wakulima kati ya lengo la tani 5,000 zilizopangwa awamu ya kwanza kufikia Agosti 31, mwaka huu.

Hayo yamebainishwa leo (01.09.2021) wakati Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Milton Lupa alipokutana na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joseph Mkirikiti ofisini kwake Sumbawanga akiwa katika ziara ya kukagua zoezi la ununuzi wa mahindi Meupe linaloendelea katika Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.

Lupa aliongeza kusema serikali inaendelea kuweka mazingira wezeshi ili kuendelea kununua mahindi ya wakulima kulingana na upatikanaji wa fedha.

“Wakala unaendelea kufuatilia fedha toka Serikalini ili itekeleze jukumu la kununua mahindi ya wakulima kama ilivyopangwa kwenye bajeti ya mwaka 2021/2022 hivyo wananchi wa Rukwa wawe na subira” alisema Lupa.

Lupa aliongeza kusema Wakala unaendelea kukamilisha ujenzi wa vihenge vya kisasa na kuwa lengo mahindi yote yatakayonunuliwa Rukwa msimu huu yahifadhiwe .

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joseph Mkirikiti alisema wananchi wa Rukwa wamezalisha kwa wingi mahindi kwa kuwa ni zao lao la biashara hivyo wanategemea zaidi NFRA kama soko la uhahika.

“Tunaendelea kuiomba serikali itupatie mgao zaidi sisi wana Rukwa kwani zao letu la mahindi ndio zao la biashara kwa wananchi wengi” alisisitiza Mkirikiti.

Kwa mujibu wa takwimu za uzalishaji wa mazao ya chakula kilimo msimu wa 2020/2021 mkoa wa Rukwa ulizalisha tani 651,433 za mahindi kati ya lengo la tani 731,500.

Mwisho.

Matangazo

  • RATIBA YA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA 2025 April 15, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 04, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • MATOKEO YA DARASA LA NNE 2024 January 04, 2025
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONGORO AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO, ARIDHISHWA NA KASI YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA UMEME

    May 05, 2025
  • JAMII YAASWA KUJENGA UTAMADUNI WA KUWAHUDUMIA WAZEE

    March 19, 2025
  • KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA TAMISEMI YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI MKOA WA RUKWA

    January 09, 2025
  • RAIS SAMIA ATOA ZAWADI ZA MSIMU WA SIKUKUU WA MWAKA MPYA KWA WATOTO YATIMA NA WENYE MAHITAJI MAALUM MKOANI RUKWA

    December 31, 2024
  • Angalia Zote

Video

LIVE- WAZIRI MCHENGERWA ANATAO TANGAZO LA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Miundombinu ya Rukwa
  • Uvuvi
  • Mikakati ya Mkoa
  • Industries
  • Madini
  • Speeches
  • Huduma za Kilimo
  • Regional History
  • Hotuba

Viunganishi Linganifu

  • Pakua Salaryslip yako hapa
  • Idara ya Takwimu (NBS)
  • Mfumo wa Kutuma, Kupokea na kufuatilia Malalamiko, Mapendekezo, Maulizo na Pongezi
  • Watumishi portal
  • Tafuta ajira Serikalini
  • Pata kila kitu kutoka serikalini

World visitors tracker

world map hits counter

Wapitiaji

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa